Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh38.2 bilioni kufikisha umeme katika vitongoji 371 Mara

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi wa usambazaji wa umeme katika vitongoji 371 mkoani humo ambao unatarajiwa kugharimu zaidu ya Sh38.2 bilioni.  Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

  • Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, utakapokamilika utaongeza idadi ya vitongoji vyenye umeme mkoani humo na kufikia 2,355 kati ya vitongoji 2,502, ifikapo mwaka 2029.

Musoma.  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatarajia kutumia zaidi ya Sh38.2 bilioni kujenga miundombinu na kusambaza umeme katika vitongoji 371 mkoani Mara, mradi utakaoanza kutekelezwa ndani ya miaka mitatu ijayo.

Mradi huo ukikamilika utaongeza vitongoji vyenye umeme kufikia 2,355 kati ya 2,502 ifikapo mwaka 2029. Kwa sasa, vijiji vyote 458 vya mkoa huo vina umeme, huku vitongoji 1,508 tayari vikiwa vimeunganishwa na 476 vikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Akizungumza Musoma leo Februari 12, 2026, Meneja Miradi wa REA Kanda ya Ziwa, Ernest Mkale, amesema mradi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuhakikisha vitongoji vyote nchini vinapata umeme ifikapo 2030. Amemtaka mkandarasi, Namis Cooperative Limited, kutekeleza kazi kwa kuzingatia mkataba.

Meneja Miradi wa Rea Kanda ya Ziwa, Ernest Mkale akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi wa usambazaji wa umeme katika vitongoji 371 mkoani humo ambao unatarajiwa kugharimu zaidu ya Sh38.2 bilioni.  Picha na Beldina Nyakeke

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, ameiagiza Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) kufikisha umeme katika migodi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ili kupunguza utegemezi wa majenereta. Amesema hadi mwaka jana migodi 34 haikuwa imeunganishwa na umeme.

Pia amemtaka mkandarasi kukamilisha mradi kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha, akionya kuwa mkoa hautavumilia visingizio vya ucheleweshaji. Aidha, ameonya dhidi ya vitendo vya kuhujumu miundombinu ya miradi.

Kwa upande wake, Meneja Miradi wa Namis Cooperative Limited, Shahidu Rutakolezibwa, ameahidi kukamilisha mradi kwa wakati, akiomba ushirikiano wa mamlaka kukabiliana na changamoto kama uhujumu na mwitikio mdogo wa wananchi kuunganishiwa umeme.