Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheikh Walid akabidhiwa rasmi ofisi, Alhad akubali yaishe

Aliyekuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akisalimiana na Sheikh Walid Omar aliyekaimu nafasi hiyo, wakati wa makabiziano ya ofisi jijini Dar es Salaam leo Februari 7, 2023. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Sheikh Walid aliteuliwa kushika nafasi hiyo Februari 2, 2023 baada ya Baraza la Ulamaa kukaa na kutengua uteuzi wa Sheikh Alhad kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa bayana.

Dar es Salaam. Siku tano baada ya kuteuliwa kuwa Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walidi Omar amekabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake, Sheikh Alhad Mussa Salum ambaye ameeleza kuridhia uamuzi uliofanywa na Baraza la Ulamaa.

Sheikh Walid aliteuliwa kushika nafasi hiyo Februari 2, 2023 baada ya Baraza la Ulamaa kukaa na kutengua uteuzi wa Sheikh Alhad kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa bayana.

Alhad aliondolewa kwenye nafasi hiyo wakati kukiwa na mjadala na malalamiko ya Dk Juma Mwaka akimtuhumu Sheikh huyo kwa kuingilia shauri lake la talaka na kutangaza kuvunja ndoa yao bila kufuata utaratibu.

Makabidhiano hayo ya ofisi yamefanyika kwenye ofisi ya Bakwata iliyopo Mtaa wa Lumumba jijini hapa, hafla ambayo imeudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Bakwata.

Sheikh Walid anamshukuru Mwenyezi Mungu na kwamba atatenda Zaidi kuliko maneno na pia ameomba ushirikiano.

“Lengo ni kufanya kazi ya Mwenyezi Mungu, hivyo naomba ushirikiano kwa viongozi wenzangu, ili tufanye kazi ambayo itaisaidia hata Bakwata,” amesema Walidi.

Kwa upande wake, Sheikh Alhad amesema ameridhishwa na maamuzi ya Baraza la kumteua aliyekuwa kaimu wake, hivyo atampa ushirikiano na zaidi ya yote amemtaka kuwa mvumilivu kwa changamoto zozote za kiofisi zitakazojitokeza.

“Sheikh Walid ni mtu sahihi na pia ni rafiki yangu mkubwa, nimekaa ofisini kwa muda mrefu nayafahamu mengi, hivyo ninaahidi kutoa ushirikiano na yeye nina imani atatusaidia akiwa kama Sheikh wa mkoa wetu,” amesema Alhad.

Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma amesema siku ya leo Februari 7, 2023 imeandikwa historia mpya kwa kufanyika makabidhiano ya ofisi ya Sheikh wa mkoa kwa amani, jambo ambalo amesema ni la kushukuru.

“Leo imekuwa historia, ofisi imekabidhiwa kwa amani na furaha ni jambo la kumshukuru Mungu,” amesema Mruma.

Katika tukio hilo, pia zimesikika sauti za waumini wa kiislamu nje ya ofisi zikimpongeza Sheikh Walidi kwa kuaminiwa na Bakwata.

Amiri Bin Omary ni mmoja wa walioudhuria shughuli hiyo, amesema yote yaliotokea ni janga, sheikh aliyeondolewa madarakani alifanya makosa kwa kutoka nje ya maadili ya kiislam, hivyo Baraza likafanya uamuzi sahihi.

“Namuomba Sheikh wetu mpya afuate maadili ya uongozi, hasa katika haki yeye na Qadhi Mkuu wanapaswa watende haki hasa katika kesi za mirathi na ndoa, washughulikie kwa usawa. Wakiona kuna ugumu basi waombe msaada kwa viongozi wa juu,” amesema Amiri

Kwa upande wake, Zainab Jaffar ambaye ni mjane amemwomba Sheikh mpya awakumbuke wajane katika uongozi wake kwani wanateseka na kuhitaji msaada.

“Namuomba Sheikh wetu mpya atukumbuke sisi wajane, hatuna mbele wala nyuma, hatuna wa kutusaidia shida zetu, tunaomba utukumbuke,” amesema Zainab.