Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yajipanga kuteka soko la ngozi

Muktasari:

Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Professa Adolf Mkenda alisema hayo juzi wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kupitia mradi unaosimamiwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), tawi la Mwanza.

Mwanza. Serikali inatarajia kuendelea kuwainua wajasiriamali wadogo, kati na wakubwa wa ngozi ili watengeneze bidhaa zinazokidhi vigezo vya kimataifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Professa Adolf Mkenda alisema hayo juzi wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kupitia mradi unaosimamiwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), tawi la Mwanza.

Alisema sekta ya ngozi ikiboreshwa itatoa fursa nyingi za ajira kwa vijana na kuchangia pato la Taifa kwa mauzo ya ndani na nje ya nchi.

“Tukiisimamia vema sekta ya ngozi, Taifa letu litaondokana na utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi ambazo baadhi ziko chini ya kiwango,” alisema Profesa Mkenda.

Alisema Tanzania inaweza kuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa za ngozi ndani na nje ya Afrika kutokana na idadi ya ng’ombe zaidi ya milioni 26 wanaofugwa nchini.

Mkuu wa DIT, tawi la Mwanza, Dk Albert Mmari alisema mafunzo kwa wajasiriamali wa ngozi yatatolewa kote nchini ikihusisha elimu kwa njia ya mitandao itakayosaidia kuwasajili, kuwaratibu na kuwafuatilia wazalishaji.

Mkurugenzi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (Sido), Omari Bakari alisema elimu ya ujasiriamali ni msingi imara katika kuongeza ubora wa bidhaa hiyo.