Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tarimba: Dawasa wanajitahidi, lakini wanatakiwa kusaidiwa

Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abbas akizungumza leo Jumanne Mei 5,2026 wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Muktasari:

  • Amezitaja Kata za Mzimumi, Tandale, Ndugumbi, Hananasifu, Makumbusho, Mwananyamala, Kigogo, Magomeni, Kinondoni na Kijitonyama.

Dodoma. Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abbas amesema Jiji la Dar es Salaam bado lina shida ya maji licha ya kazi kubwa inayofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Dawasa).

Amesema Dawasa kupitia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Mkama Bwire wamekuwa wakipambana kuhakikisha wananchi wanapata mjisafi na salama.

Abbas ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 5,2026 wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ambapo ametaja maeneo yenye changamoto kubwa ya maji.

Tarimba amezitaja kata za Mzimumi, Tandale, Ndugumbi, Nanasifu, Makumbusho, Mwananyamala, Kigogo, Magomeni, Kinondoni na Kijitonyama.

Hata hivyo, Tarimba amesema kuwa Dawasa inahitaji kusaidia ili iweze kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwa mahitaji ya maji ni makubwa.

"Maji yanayotakiwa Dar es Salaam ni zaidi ya lita 772 milioni kwa siku, lakini yanayozalishwa ni lita 553.7 milioni kwa siku ambapo upungufu ni lita 259 milioni. Dawasa wanafanya kazi kubwa, lakini bila kusaidiwa itakuwa uongo," amesema Abbas.

Pia, amesema maji yanayozalishwa hayafiki yote katika Jiji hilo lenye idadi kubwa ya wakazi kwa kuwa, bado kuna changamoto ya upotevu wa maji.

Amesema asilimia 49 ya maji yanayozalishwa yanapotea kutokana na kuchoka kwa mitambo ingawa, amesema ipo mitambo mipya imepelekwa lakini ufungaji wake unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2026.

Kutokana na hilo, Tarimba amependekeza utengenezwe utaratibu wa jinsi ya kuondoa upotevu wa maji angalau kwa ufikie asilimia 25.

Kwa mujibu wa Abbas, mitambo inayosukuma maji Dar es Salaam ni ya tangu 1960 na mingine imejaa kutu kutokana na kukaa muda mrefu akaomba zikopwe fedha ili kuibadilisha.

Amesema maji ni dini, siasa, maisha na kila kitu kitu akitumia kauli ya Waziri Aweso kuwa maji hayana mbadala.

Kuhusu Bwawa la Kidunda amesema mradi umeanza 2023, lakini hadi sasa ni asilimia 47 wakati imebaki miezi minane akihofu huenda kazi haitakamilika.