Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taso wapeleka kilio kwa Rais Samia wakitaka uwanja wao wa Themi Arusha

Kaimu Mwenyekiti wa TASO, Jovin Ndimbo

Muktasari:

Chama cha Wakulima Tanzania (Taso) kimemwangukia Rais Samia Suluhu Hassan kuomba awasaidie kuwarudishia uwanja wa Themi wa Arusha ambao sasa uko mikononi kwa Jiji.

Dodoma. Chama cha Wakulima Tanzania (Taso) kimemwangukia Rais Samia Suluhu Hassan kuomba awasaidie kuwarudishia uwanja wa Themi wa Arusha ambao sasa uko mikononi kwa Jiji.

 Uwanja wa Themi umekuwa kwenye mvutano kutokana na kinachoelezwa kuwa Taso hawakuwa wamelipia gharama zilizotakiwa kulipwa wakati wanaomba kuumiliki na hivyo kuwepo na deni kubwa kutoka kwa mmiliki wa awali na malimbikizo ya kodi ya ardhi.

Taso wamekutana jijini Dodoma kuzungumzia jambo hilo wakiwashirikisha kamati ya Rais inayohakiki mali ambao walisaidia kuwapa ukweli na namna uhakiki wao ulivyobaini mapungufu kwenye umiliki wa uwanja huo kutoka kwa wamiliki wa awali.

Kaimu Mwenyekiti wa Taso, Jovin Ndimbo amesema mzozo kuhusu uwanja huo zilianza siku nyingi lakini hali ilipofikia kwa sasa wanaomba kiongozi mkuu wa nchi kutumia nafasi yake kwa ajili ya kuwasaidia kuurudisha.

Ndimbo amesema Jiji la Arusha walishawaandikia barua ya kuuchukua uwanja huo kwa madai kuwa uwanja huo ni mali yao na kwamba Taso pia wanadaiwa deni kubwa ambalo lilitokana na kutolipa fidia ya kuutwaa uwanja wao na malimbikizo ya kodi ya ardhi.

Amesema haamini kama madai hayo yapo kwao isipokuwa anataja mgogoro baina yao ulianzia mwaka 2017 baada ya Serikali kutaka Taso wasisimamie maonyesho ya wakulima nanenane na kutakiwa wakabidhi viwanja vyote licha ya kuwa ndani ya viwanja hivyo kuna majengo na mali zao.

“Ndugu zangu, hapo ndipo mgogoro ulipoanzia, baadhi ya viwanja wenyeviti wa mikoa walikuwa wanaitwa kibabe na kuambiwa haraka kabidhi hata bila ya kufuata taratibu, sasa leo tumeanza kugeukwa tena na baadhi ya mali zetu ikiwemo Themi ndiyo tunaelezwa kuwa si mali yatu,” amesema Ndimbo.

Hata hivyo maelezo kutoka kamati ya Rais yanaonyesha kuwa Taso licha ya kukabidhiwa uwanja wa Themi 1993, lakini haikuwahi kulipa fidia kama ilivyotakiwa na hivyo deni la uwanja huo kuongezeka zaidi lakini wakabainisha kuwa kama watakamilisha baadhi ya mambo, wanaweza kukabidhiwa.

Ofisa kutoka ofisa Rita, Joseph Jackson amewataka Taso kuwa na utaratibu wa kuzitambua mali zao kwa kupitia kwadhamini wao lakini akataka wafuate taratibu zinazotakiwa.

Jackson amesema Rita inaitambua bodi ya wadhamini wa Taso kwamba ipo kihalali kwa hiyo wanatakiwa kusimamia mali na madeni kwa kufuata taratibu za kisheria kama zinavyotaka.