Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TCAA , Precision kuchunguza ndege Zanzibar

Muktasari:

Tukio hilo lilitokea Juni 16 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karume mjini Zanzibar.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakishirikiana na mafundi wa Kampuni ya Ndege ya Precision wameelekea Zanzibar kuchunguza tukio la ndege ya kampuni hiyo kupata hitilafu na kuwaka moto na kusitisha safari.

Tukio hilo lilitokea Juni 16 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karume mjini Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Mawasiliano wa Prescion Air, Azda Mkullo inasema wamepeleka injini mbadala kwa ajili ya kufungwa.

Inaongeza kuwa baada ya tukio hilo ilimlazimu rubani kuchukua hatua za kuuzima moto na kuirudisha  ndege kwenye eneo la maegesho.