Tigo yazungumzia huduma za fedha kutofanya kazi

Wednesday April 07 2021
tigopic
By Aurea Simtowe

Dar es Salaam. Wakati watumiaji wa huduma za kifedha kupitia kampuni ya  mawasiliano ya simu ya Tigo wakilalamikia kukosa huduma kwa saa kadhaa, mtandao huo umesema kuna tatizo la kiufundi na linafanyiwa kazi.

Watumiaji hao wamepaza sauti zao leo Jumatano Aprili 7, 2021  kupitia mitandao ya kijamii hasa  Twiiter wakihoji juu ya ugumu wanaokutana nao wanapotaka kufanya miamala.

“Shida nini mbona hatuwezi kupata ‘access’ ya Tigopesa na mpo kimya,” meandika [email protected]

[email protected] aliandika “tunaomba mfanye marekebisho ya mtandao jioni kwa sababu watu wanashindwa kutoa hela zao.”

Mdundo Victor @masivu_12 amesema, “huduma toka jana hazipatikani mbona hamtoi taarifa.”

Woinde Shisael ambaye ni meneja mawasiliano wa kampuni hiyo ameieleza Mwananchi Digital kuwa tatizo hilo lipo,  “ni kweli kuwa huduma yetu ya Tigo pesa haipatikani kwa sasa kwa sababu ya tatizo la kiufundi. Wataalamu wetu wanafanyia kazi tatizo hili na tutakujulisha pindi huduma itakaporejea. Hata hivyo wateja wetu wamejulishwa hili.”

Advertisement

Licha ya Shisael kusema hayo na taarifa hiyo kuchapishwa katika ukurasa wao wa Twitter, baadhi ya watu waliendelea kuhoji kuwa ni kwa nini taarifa haikutolewa mapema.

“Nyie mnazingua sana, hii imeanza kuanzia jana hadi leo na hamkutoa taarifa yoyote mnatuchukuliaje,” amesema Nsinda nsinda @NNsinda kupitia ukurasa wake wa Twitter huku

Peter Bundallah akisema, “kama kuna maboresho au marekebisho muwe mnatoa taarifa mapema ili turekebishe mambo yetu kuliko kutupa shida kiasi hiki.”


Advertisement