Tukio kubwa la kimataifa la KAIZEN lafanyika jijini Dar es Salaam

Majadiliano yaliyohusisha wajumbe wanane kuhusiana na uongezaji kasi shughuli za KAIZEN.
Muktasari:
- Mkutano wa nne wa mwisho wa mwaka wa KAIZEN Afrika (AKAC 2021) ulifanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency, Dar es Salaam kuanzia Agosti 24 mpaka 26, 2021.
Mkutano wa nne wa mwisho wa mwaka wa KAIZEN Afrika (AKAC 2021) ulifanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency, Dar es Salaam kuanzia Agosti 24 mpaka 26, 2021.Mkutano uliandaliwa kwa pamoja baina ya Wizara ya Viwanda na Biashara, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japan (JICA).Mkutano wa AKAC, tangu mwaka 2018, umekuwa ukiandaliwa kila ifikapo mwisho mwa mwaka kama tukio kubwa lenye hadhi ya kimataifa kwa ajili ya KAIZEN Afrika ukiwa na lengo la kubadilishana maarifa na uzoefu baina nchi na kusambaza falsafa za KAIZEN katika bara zima la Afrika.Kwa Tanzania, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuendesha mkutano mkubwa kama huu katika mtindo wa kuchanganya hadhira mbili tofauti (wale wanaoshiriki moja kwa moja na wale wanaoshiriki mtandaoni) hii yote ni kwa sababu ya tishio la ugonjwa wa Uviko-19.

Zaidi ya Watanzania 130 walishiriki moja kwa moja ukumbini Hyatt Regency na zaidi ya washiriki 700 kutoka katika nchi zaidi ya nchi 20 walijiunga na mkutano huo kwa njia ya mtandao.Wakati wa mkutano huo, shughuli za KAIZEN za Tanzania zilitambulishwa kwa nchi zingine kwa mfululizo wa vipindi.Uwasilishaji wa mfano wa KAIZEN Tanzania – kesi ya kwanza ya utekelezaji wa shughuli za KAIZEN kwa upande wa kongano la viwandaShughuli za KAIZEN zimetekelezwa katika nchi zaidi ya 10 za Afrika tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kwa Tanzania, Wizara ya Viwanda na Biashara na Jica wamekuwa wakitekeleza kwa pamoja mradi ujulikanao “Uimarishaji Viwanda vya Kati kupitia Uboreshaji wa Tija na Ubora (KAIZEN),” tangu mwaka 2013. Tanzania ndiyo nchi ya kwanza kwa Afrika kutekeleza mpango wa KAIZEN kwa kutumia kongano kwa maendeleo ya viwanda. Pia inajulikana kama “Mfumo wa KAIZEN wa Tanzania” na mfumo huo ulitambulishwa kwa nchi zingine za kiafrika katika siku ya pili ya mkutano huo. Mradi huo ulichagua kongano la viwanda vitatu (yaani kongano la viwanda vya zabibu huko Dodoma, kongano la viwanda vya uhandisi chuma mkoani Morogoro, na kongano la viwanda vya mpunga Mbeya) na kundi jingine jipya lililoko Kagera ambaloni kongano la kampuni ndogo zaidi ya 100 ambazo zimechukuliwa kama sehemu ya majaribio na waliweza kutumia mpango wa shughuli za KAIZEN kwa kampuni za kongano hilo mwanzoni mwa mwaka 2020. Kulingana na uwasilishaji, takriban asilimia 70 za kampuni zinazoshiriki zimepata mafanikio makubwa katika upande wa muda wa kuwasilisha bidhaa za wateja kwa wakati muafaka, uokoaji muda wa utafutaji bidhaa, utengenezaji nafasi kupitia shughuli za KAIZEN.Majadiliano yaliyokutanisha wajumbe 8 kuhusu uongezaji kasi wa utekelezaji wa mpango wa KAIZENMajadiliano hayo yalisimamiwa na Katibu wa Tawala wa zamani wa Mkoa wa Dodoma, Paul Maduka Kessy na kuwasilishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, Dar es Salaam, Dk Edwin P. Mhede na wawasilishaji wengine saba.Washiriki wa majadiliano hayo walijadili kuhusu “Kuongeza kasi ya Maendeleo ya Viwanda kupitia KAIZEN nchini Tanzania”.Wajumbe walihitimisha majadiliano kwa kuangazia umuhimu wa uongozi wa juu, teknolojia, ushiriki wa sekta binafsi, na kutekeleza sera za kuongeza kasi zaidi.Mabanda ya viwanda mbalimbali kwa ajili ya kutambulisha shughuli zao za KAIZENKampuni nne zinazowakilisha kampuni zingine ambazo zinatekeleza shughuli za KAIZEN nchini Tanzania ziliweka mabanda yao huko Hyatt Regency na kuonyesha bidhaa zao wakati wa mkutano wa AKAC. Walitambulisha bidhaa zao na shughuli za KAIZEN kwa washiriki na vyombo vya habari.Namna gani tunaweza kutekeleza mpango wa KAIZEN?Mpango wa RuzukuZaidi ya Wakufunzi 100 wa KAIZEN wamethibitishwa na Wizara ya Viwanda na Biashara nchini, na wanaweza kutoa huduma za ushauri kuhusiana na KAIZEN kwa viwanda na kampuni mbalimbaliHuduma hizo ni za kulipia, lakini Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo nchini (SIDO) linatekeleza mpango wa ruzuku kwa ajili ya kupeleka wakufunzi wa KAIZEN katika maeneo lengwa ifikapo tarehe 31 Oktoba, 2021.Namna ya kujifunza KAIZEN kupitia mtandaoniJica iliboresha (ilisasisha) vifaa vya video ambavyo hutumiwa bila malipo ili kujifunza KAIZEN Agosti 2021 na kuzitangaza kupitia mtandao wa YouTube.Uliwekwa utaratibu wa vipindi 3 kama ifuatavyo. Ikiwa una nia, tafadhali jiunge nasi!Unaweza kupata msimbo kutoka katika jedwali liliopo chini.Mustakabali wa shughuli za KAIZEN nchiniKAIZEN inamaanisha “Uboreshaji endelevu”. Mkutano wa AKAC wa mwaka 2021 ulihitimishwa, lakini falsafa ya KAIZEN bado inaendelea.Wizara ya Viwanda na Biashara imepanga kutekeleza shughuli za KAIZEN kwa wafanyabiashara wapatao 1,500 wa Kitanzania ifikapo mwaka 2030 kulingana na sera yao inayoitwa “Mfumo wa Uboreshaji wa Ubora na Tija (KAIZEN) katika sekta ya viwanda 2020- 2030” (FKM 2020-2030).Kwa kuongezea, mwaka ujao wa 2022, Mkutano wa 8 wa Tokyo juu ya Maendeleo ya Afrika (TICAD8) utafanyika Tunisia, na viongozi wa kisiasa (ikiwamo wakuu wa nchi) kutoka nchi za Afrika na Japan watakutana na kubadilishana mawazo juu ya maendeleo ya Afrika.KAIZEN pia itajadiliwa katika mkutano wa TICAD8 kama eneo muhimu kwa viwanda vya Afrika. Inatarajiwa kwamba Tanzania inaweza kupata maendeleo zaidi na kuboresha mpango wake wa KAIZEN kwa nchi zingine za Kiafrika na Japan katika TICAD8 ijayo.KAIZEN ni nini?“KAIZEN” ni neno lenye asili la Kijapani linalomaanisha “Uboreshaji endelevu”, na falsafa ya usimamizi na ujuzi wa uendelezaji wa ubora na tija wa taasisi lengwa. Pia ni mkakati uliotanguliza maslahi ya binadamu mbele, unaokuza umoja, mabadiliko ya fikra, kujitegemea, ubunifu, na busara ya kupata mawazo ya wengine katika kutafuta suluhisho la changamoto tunazokabiliana nazo nchini. “Maendeleo ya Viwanda ya kongano” ni njia ambayo inakusudia kuchagiza ajenda ya viwanda kwa kutumia faida ya ukusanyaji pamoja, uwekaji katika makundi kijiografia wa kampuni zenye mahusiano ya moja kwa moja na taasisi washirika katika uwanja eneo fulani. Kuhimiza ushiriki wa nguvu taasisi na kampuni zinazohusika karibu na minyororo ya thamani, na kushawishi ushirikiano kati yao ambao husaidia kukuza ubunifu na viwanda vya ndani.Kuhusu JICAShirika linalosimamia misaada ya nchi ya Japani.Ni moja wapo ya mashirika makubwa zaidi ya misaada ya ulimwengu yanayosaidia maendeleo ya uchumi katika nchi zinazoendelea ulimwenguni.Hapa nchini, Jica imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Tanzania kwa takriban miaka 60 katika sekta nyingi kama vile kilimo, viwanda, miundombinu, nk tangu mwaka 1962.