Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tumbaku za Sh500 bilioni zanunuliwa

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora. Pcha na Robert Kakwesi

Muktasari:

Kilo 104 milioni za tumbaku zenye thamani ya Sh500 bilioni zimenunuliwa hadi sasa katika masoko ya tumbaku yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini.

Tabora. Kilo 104 milioni za tumbaku zenye thamani ya Sh500 bilioni zimenunuliwa hadi sasa katika masoko ya tumbaku yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini.

Kilo zilizonunuliwa ni sawa na asilimia 86.6 ya tumbaku ambayo imelengwa kununuliwa msimu huu ambayo ni kilo 120 milioni.

Akifunga maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani (SUD), yanayofanyika Kitaifa mkoani Tabora leo Julai Mosi 2023, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema ana uhakika lengo litafikiwa la kununuliwa kilo 120 milioni.

Amebainisha kuwa kati ya tumbaku iliyonunuliwa yenye thamani ya zaidi ya Sh500 bilioni tayari kampuni zimelipa Sh400 bilioni na zinadaiwa Sh100 bilioni.

Ameeleza kuwa msimu uliopita wakulima waliuza kilo 60 milioni na kwamba waliweka makubaliano ya kufikia kilo 120 milioni msimu huu ambazo zitafikiwa.

“Tumekuwa na ongezeko hilo na nina amini tutalifikia masoko yatakapofikia mwisho msimu huu,” amesema

Amesema kumekuwa na changamoto ya baadhi ya kampuni kuwalipa wakulima na kudai atakutana na mabenki, kampuni ya ununuzi wa tumbaku na viongozi wa vyama vya ushirika kujadiliana changamoto ya malipo kwa wakulima.

Waziri Bashe amesema mwaka huu wanavunja rekodi kwa bei ya wastani kwa kilo ambapo hadi sasa ni Dola 2.3, akisema na wengine wameuza zaidi ya wastani huo.

Awali Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku, Hassan Wakasuvi, ameeleza baadhi ya kampuni kushindwa kuwalipa wakulima kwa wakati na kuwafanya wazidai kampuni hizo baada ya kuuza tumbaku yao.

Alimuomba Waziri Bashe, kuwafikiria wakulima hao na kuangalia namna watakavyolipwa kutokana na jasho lao.

Maadhimisho hayo yalifunguliwa Juni 27, 2023 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde, yakiwa yanafanyika Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo mkoani Tabora.