Ubalozi wa Marekani kuadhimisha siku ya Kiswahili Duniani Dar

Muktasari:

  • Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco) lilitangaza Julai 7 kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili Duniani, mwaka huu ni mara ya pili maadhimisho hayo kufanyika duniani kote.

Dar es Salaam. Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania unatarajia kufanya maadhimisho ya Kiswahili katika ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2023.

Mgeni maalumu katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita), Consolata Mushi.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo, maadhimisho hayo yatayayofanyika kwenye ofisi za ubalozi yanatarajiwa kufanyika kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 10:30 jioni.

Washiriki wa mdahalo huo watakuwa ni Kituo cha Mafunzo cha MS TCDC Arusha, wafanyakazi, wanafunzi wa Kiswahili wa Ubalozi wa Marekani, Shirika la Wamarekani wa Kujitolea (Peace Corps).

Pia, maadhimisho hayo yatawashirikisha wanaharakati wa lugha ya Kiswahili, Joram Nkumbi, Abdul Fumau ambaye ni mshairi chipukizi pamoja na Seko Shamte anayejishughulisha na kutayarisha filamu.

Mada itakayojadiliwa katika kongamano hilo ni ‘Kiswahili kinavyoimarisha Uhusiano wa Kiuchumi na Kiutamaduni kati ya Tanzania na Marekani.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa maadhimisho ya Kiswahili duniani ambayo kilele chake kitafanyika Zanzibar, Julai 7, 2023.