Upelelezi mauaji mfanyabiashara madini wakamilika
Mtwara. Faili la kesi ya mashtaka ya mauaji ya mauaji ya Mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis , inayowakabiri maafisa saba wa polisi lahamishiwa Mahakama kuu Kanda ya Mtwara, baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Charles Mnzava amesema leo Ijumaa Mei 5, 2023 kuwa upelelezi umeonyesha kuwa washitakiwa wote saba wanakabiliwa na kesi.
Amesema siku ya Alhamisi Mei 4, 2023 ilielezwa na upande wa Mashtaka kupitia Mkuu wa Mashtaka, Joseph Mauggo mahakamani hapo kuwa upelelezi umekamilika hivyo walisomewa ‘committal proceedings’ wakijulishwa kwamba upelelezi umekamilika hivyo kesi inahamishiwa mahakama kuu ikiwa pamoja na taarifa za vilelezo na mashahidi.
Upande wa mashtaka unakusudia kuwasilisha mahakamani zaidi ya mashahidi 70, vielelezo vya maandishi visivyopungua 31 na vielelezo vinavyoonekana vitano.
"Sisi tumemaliza kwa hiyo hawatoletwa tena hapa Mahakama ya mkoa kesi inaenda kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara.
Maafisa saba wa polisi walifikishwa kwa mara ya kwanza Mahakamani hapo Januari 2022 kwa shitaka la mauaji ya Mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis Hamis ( 25), Mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.
Mauaji hayo yanadaiwa kutokea Januari 5, 2022 mkoani hapa
Washitakiwa hao ni pamoja na aliyekuwa Mrakibu wa polisi na Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje, Mrakibu Msaidizi wa polisi aliyekuwa Mkuu wa kituo cha polisi Mtwara, Charles Onyango, Mrakibu wa polisi aliyekuwa Mkuu Intelijensia mkoa, Nicholaus Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya, Mkaguzi msaidia wa polisi, Marco Mbuta, Mkaguzi wa polisi Shirazi Ally Mkupa na askari namba G5158 Kopro Salum Juma Mbalu.