Ushauri kwa vijana waliomaliza mafunzo ya JKT

Sunday December 13 2020
JKT PIC

Kibondo. Vijana nchini Tanzania wametakiwa kuwa na nidhamu ya maisha ili kujiepusha na magonjwa yatakayosababisha washindwe kujikwamua kiuchumi.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Desemba 13, 2020 na mkuu wa kikosi cha 824 Kanembwa JKT, Luteni Kanali Shija Sahani wakati wa kufunga mafunzo ya awali  Jeshi la Akiba la Mgambo  katika kijiji cha Bitulana Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma.

Amesema vijana wengi kwa sasa wanashindwa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa kuendekeza ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.

Amebainisha kuwa kupima afya na kujilinda na maambukizi ya magonjwa ni jambo muhimu ili kujua afya na kuendelea kuwa imara, “sasa nyinyi mlihitimu mafunzo ya kijeshi mmejifunza mambo mengi na kitendo cha kuwakutanisha kwa pamoja najua kitakuwa kimewaletea mabadiliko na mmefundishwa mambo mengi mnatakiwa kuwa chachu kwa vijana wenzenu popote mtakapokuwa kwa kuwashauri,”

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo, Joynes Mkela na Dikson Chubwa wameeleza jinsi vijana wanavyojisahau katika masuala mbalimbali, kuahidi kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.

Mafunzo hayo yalianza Julai 17, 2020 na vijana 298 wavulana wakiwa 276 na wasichana  22  huku 121 wakishindwa kumaliza mafunzo na kati yao wavulana 112 na wasichana tisa.

Advertisement
Advertisement