Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utelekezaji wa wa watoto wakithiri Wilaya ya Mwanga

Wadau wa kutetea haki za binadamu kutoka shirika lisilo la kiserikali la  Ajiso mkoani Kilimanjaro wakijadili namna ya kukabiliana na matukio ya ukatili kwenye jamii.Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Vitendo vya baadhi ya wazazi katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kuwaacha watoto mikononi mwa bibi na babu zao, kumetajwa kuchangia ukatili wa kijinsia kwa watoto kutokana na wazee hao kukosa muda wa kuwahudumia.

Mwanga. Vitendo vya baadhi ya wazazi katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kuwaacha watoto mikononi mwa bibi na babu zao, kumetajwa kuchangia ukatili wa kijinsia kwa watoto kutokana na wazee hao kukosa muda wa kuwahudumia.

Hayo yamebainishwa leo na Ofisa Sheria wa Shirika la Kisheria na kutetea haki za binadamu (Ajiso), Tatu Mrutu wakati akitoa elimu kwa jamii ya namna ya kupambana na matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto.

"Sasa hivi kumekuwa na wimbi la baadhi ya wasichana kuzaa watoto na kuwatelekeza kwa mama zao na watoto hawa wakati wakilelewa na bibi zao hawaangaliwi vizuri na wakati mwingine wanapata vishawishi na kurubuniwa au kufanyiwa matukio ya udhalilishaji ikiwemo ukatili wa kijinsia," amesema.

Ameendelea kusema kuwa tabia ya wanawake kutelekeza watoto wao na kuacha walelewe na bibi zao imekuwa ni changamoto.

“Wanawake wanawaacha mtoto wao wanakwenda kutafuta maisha na wakati mwingine hawarudi nyuma kuangalia kama watoto wao wanalelewa vizuri au la," amesema Tatu.

Aidha amesema kutokana na vitendo hivyo kukithiri kwenye jamii wameamua kutoa elimu kwenye jamii ili kuangalia namna ya kukabiliana na tatizo hilo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa jamii.

Abdi Msangi ambaye ni mkazi wa Kata ya Kirongwe wilayani Mwanga, amesema zaidi ya asilimia 60 watoto waliopo mtaani ni wale ambao wametelekezwa na wazazi wao ambao wakati mwingine hufanyiwa vitendo vya ukatili.

"Matukio ya ukatili ambayo mara nyingi yanafanywa na vijana huku mtaani yanawakumba zaidi watoto ambao wametelekezwa na wazazi wao na wanaishi na bibi zao, kutokana na kwamba hawana muda wakuwaangalia wajukuu zao ambapo wakati mwingine wanafanyiwa vitendo vya kikatili," amesema.