Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: 18 wanusurika kifo ajali wachezaji Polisi Tanzania

Majeruhi ajali ya wachezaji Polisi Tanzania watajwa

Muktasari:

  • Wachezaji 18 wa timu ya Polisi Tanzania waliokuwa wakitoka mazoezini katika viwanja vya TPC  Wilaya ya Moshi  mkoani Kilimanjaro wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia na  kugonga mti eneo la Mkababuni kata ya Arusha chini.

Moshi. Wachezaji 18 wa timu ya Polisi Tanzania waliokuwa wakitoka mazoezini katika viwanja vya TPC  Wilaya ya Moshi  mkoani Kilimanjaro wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia na  kugonga mti eneo la Mkababuni kata ya Arusha chini.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema  ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Julai 9, 2021 na kubainisha kuwa gari hilo lilikuwa na watu 32 wakiwemo makocha, madaktari na wachezaji hao.

Amesema waliojeruhiwa zaidi ni mchezaji  Gerald Mathias ambaye amevunjika miguu yote miwili pamoja na dereva wa gari hilo,  Vicent Ngonyani aliyevunjika mbavu moja.

Amebainisha kuwa majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwa ajili ya matibabu na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa.

New Content Item (1)
18 wanusurika kifo ajali wachezaji Polisi Tanzania

Ofisa uhusiano msaidizi wa hospitali ya KCMC, Joel Masawe amesema waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu na dereva yupo katika chumba cha uangalizi maalum.