VIDEO: Baba asimulia mwanaye alivyojinyonga baada ya Simba kufungwa na Yanga
Muktasari:
- Kufungwa kwa Simba bao 1-0 na Yanga Uwanja wa Mkapa kumeacha maumivu makali katika familia ya Joseph Edward na mkewe Magdalena Patrick baada ya mtoto wao Joshua (9) kujinyonga akichukizwa na matokeo hayo.
Dar es Salaam. Kufungwa kwa Simba bao 1-0 na Yanga Uwanja wa Mkapa kumeacha maumivu makali katika familia ya Joseph Edward na mkewe Magdalena Patrick baada ya mtoto wao Joshua (9) kujinyonga akichukizwa na matokeo hayo.
Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Goroka B, uliopo kata Toangoma siku Julai 3, 2021 saa 2 usiku. Mtoto huyo alikuwa anasoma Shule ya Msingi ya Upendo.