Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Ndugai adai kuwatambua kina Mdee, kuwapangia kazi za kibunge

VIDEO: Ndugai adai kuwatambua kina Mdee, kuwapangia kazi za kibunge

Muktasari:

Amesema wabunge hao wataendelea na shughuli zote za kibunge, labda wakijiuzulu wenyewe.

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema bunge litaendelea kuwatambua wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema na wataendelea na shughuli zote zinazohusu mhimili.

Ndugai ameyasema hayo leo wakati wa kuwaapisha wabunge wateule Riziki Lulida na Humprey Polepole katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya bunge.

Spika Ndugai pia ameweka wazi kuwa wabunge hao watakuwa sehemu ya kamati za Bunge anazotarajiwa kuziunda hivi karibuni na watashiriki shughuli zote za bunge.

“Wabunge wote wa bBunge la 12 tuliowaapisha tunaendelea kuwatambua kwamba  ni wabunge kamili ikiwa ni pamoja na wale   wa Chadema akiwamo Aida Khenani. Nashangaa wanawasonga tu hawa 19 yule mmoja vipi, wakiweza wamfukuze lakini sisi tumeshamuapisha na tunamtambua kwamba ni mbunge.

Niwahakikishie wale 19 ni wabunge kamili labda wao wenyewe kwa kutumia utaratibu wa kikatiba waamue kujiuzulu, ila hivi karibuni nitaunda kamati na watakuwa sehemu ya kamati hizo,” amesema Spika Ndugai.