VIDEO: Sababu za Mrema kutaka kuoa

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema ameelezea kilichomsukuma kuoa kuwa ni pamoja na kuepuka matamanio na kuzini kwa macho.
     

Moshi. Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema ameelezea kilichomsukuma kuoa kuwa ni pamoja na kuepuka matamanio na kuzini kwa macho.

Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urais wa Tanzania, ameyasema hayo jana Machi 21,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake katika kijiji cha Kiraracha, wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema baada ya mke wake kufariki mwaka jana alibaki mpweke na kutokana na hali yake ya kiafya akaona ni vyema kumtafuta mwenza ambaye atamhudumia na kumtunza na kwamba tayari amepata baraka zote za familia pamoja na kanisa na Mungu akipenda atafunga ndoa alhamisi ya machi 24, mwaka huu.