Vijana wilayani Siha wadaiwa kwenda kwenye misiba wakiwa wamelewa

Tuesday June 28 2022
ulevipiic
By Bahati Chume

Siha. Mkuu wa Walaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Thomas Apson amewataka vijana wilayani humo kuacha kwenda kwenye misiba wakiwa wamelewa pombe kwa maelezo kuwa si uungwana.

Ameeleza  hayo leo Jumatatu Juni 27, 2022 katika mashindano ya West Kili Forest Tour Challenge yalifanyika katika viwanja vya Simba Farm West Kilimanjaro.

Amesema amelazimika kuzungumza hayo baada ya kupata taarifa kutoka kwa viongozi wa dini wilayani humo kwamba baadhi ya vijana  wanatabia ya kufika kwenye msiba wakiwa wamelewa.

‘’Ni kweli viongozi wa dini wamenipa taarifa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama ya wilaya nipaze sauti kuhusu tatizo hili, vijana waache mara moja tabia hiyo, wanakuja wamelewa hata kuchimba kaburi na kufukia ni tatizo, lazima tulinde vijana kwani ni nguvu kazi ya Taifa, ‘’amesema Apsoni.

Amebainiasha kuwa alishuhudia vijana wakifukia kaburi wakipepesuka na wengine wakirusha matawi ya mgomba na kumkosakosa  yeye na mkuu wa polisi wa wilaya katika mazishi ya kijana mmoja eneo la Fuka.

Mbali na hilo amesema anatarajia kukutana na kampuni za utalii kutoka sehemu mbalimbali ikiwamo Mkoa wa Arusha kujadili namna ya kufungua frusa ya ajira kwa vijana wa wilaya hiyo  ya kupandisha watalii Mlima Kilimanjaro.

Advertisement

"Ni kweli hawapati fursa ya kupanda na wageni kuwaonyesha mlima Kilimanjaro lakini cha ajabu na kinachasikitisha kampuni za mikoa ya jirani zinakuja na watu wao, hivyo kuwanyima wenyeji fursa hiyo," amesema.

Deogratus Martin, kiongozi kutoka mradi wa Sauti chini ya World Vition, amesema mashindano hayo ni mazuri kwani yanautangaza utalii ‘na  wapo bege kwa bega kuhusu utalii huo na pia kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa watu wote kwa lengo la kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi

Meneja wa shamba la miti West Kilimanjaro (TFS), Yahaya Masawanga amesema madhumuni ya kuadhisha West  Kili Forest Tour ni kuhamasisha vivutio vya  mbalimbali vya utalii vilivyopo wilayani humo

Advertisement