Vikundi 55 vyapata mkopo Sh96 milioni Sengerema

Thursday November 25 2021
mkopopic
By Daniel Makaka.

Sengerema. Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza imetoa mkopo wa Sh96 milioni kwa vikundi 55 vya akina mama, vijana na wenye ulemavu.

Akikabidhi mkopo huo leo Alhamisi  Novemba 25, 2021 Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Binuru  Shekidele amesema mikopo hii itumike kwa kuinua maisha yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwaa la akina mama katika wilaya hiyo, Daline Matonange ametoa ushauri kwa Halmashauri ya Sengerema kutoa mikopo kwa kusaidia uanzishwaji viwanda katika wilaya hiyo.

Amesema mikopo hii ikitolewa kwa vikundi imara vitasaidiwa  kuanzisha viwanda vidogo vidogo hali itakayosaidia vijana kujikwamua kimaisha.

Kwa upande wake ofisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Sengerema, Abel Mosha amesema kwa sasa wamejipanga kutoa mikopo kwa vikundi vichache Ili viweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo .


Advertisement
Advertisement