Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wakuu wa Serikali kuongoza kampeni ya usafi wa mazingira nchi nzima

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira), Dk Seleman Jafo

Muktasari:

  • Kaulimbiu ya mwaka huu 'Urejeshwaji wa Ardhi, Ustahilimivu na Hali ya Jangwa na Ukame' inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za makusudi  kuhimiza matumizi endelevu ya ardhi ikiwa ni moja ya nguzi muhimu ya kutunza na kuboresha mifumo ya ikolojia mbalimbali na ustawi wa viumbe hai.

Dar es Salaam. Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Serikali imetangaza kampeni ya usafi wa mazingira nchi nzima itakayoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Philip Mpango.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Seleman Jafo amesema hayo leo Mei 27,2024 na waandishi wa Habari  wakati wa  kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayotarajiwa kufanyika  kitaifa jijini Dodoma Juni 5, 2024.

Jafo amesema kampeni ya usafi itafanyika Juni Mosi ambapo Dk Mpango ataongoza usafi huo Jiji Dar es Salaam wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ataongoza katika Kanda ya Ziwa Hospitali ya Kanda Chato mkoani Geita.

"Ninawaomba wananchi siku ya Juni Mosi mwaka huu ni siku ya usafi nchi nzima hivyo mnatakiwa kufanya usafi kwenye maeneo yenu ili kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo yatafanyika Juni 5 mwaka huu," amesema Dk Jafo.

Jafo amesema kwa upande wa Kanda ya Kati Dodoma kampeni ya usafi itaongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati, Doto Biteko na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoa wa Mbeya atakuwa Spika wa  Bunge, Dk Tulia Ackson.

Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kampeni ya usafi utaongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma pamoja na mikoa mingine itasimamiwa na wakuu wa mikoa husika.

Amesema kutokana na kuwepo Kwa changamoto za uharibifu wa ardhi pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi kaulimbiu itakayoongozwa maadhimisho hayo kitaifa ni 'Urejeshwaji wa Ardhi, ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame'.

Dk Jafo amesema Mei 31 mwaka huu kutakuwa na kongamano la kitaifa la wadau wa mazingira litakaloongozwa na Makamu wa Rais, Dk Mpango watakaoshiriki ni  wataalamu wa mazingira na sekta mbalimbali kutoka wizarani na serikalini.

Kuanzia Juni Mosi hadi Juni 6 mwaka huu kutakuwa na maonyesho ya wiki ya mazingira ambapo wadau mbalimbali watapata fursa ya kuonyesha teknolojia, uvumbuzi na ubunifu wa masuala mbalimbali yanayohusu hifadhi na usimamizi wa mazingira ambayo yatazinduliwa na Makamu wa Rais, Dk Mpango jijini Dodoma.

Dk Jafo amesema siku hiyo Makamu huyo pia atazindua sera ya Taifa ya Uchumi wa Bluu na mkakati wa utekelezaji wa sera mwaka 2024.

Amesema nchi ya Tanzania Ina utajiri wa rasilimali katika maji bahari na maji baridi zinazojumuisha kilometa za mraba 61,500 za maeneo ya maji baridi yanayofaa kwa matumizi mbalimbali pamoja na kilometa 64,000 za maji kitaifa katika  bahari na kilometa za mraba 223,000 za ukanda maalumu wa uchumi wa bahari .

Vilevile nchi Ina ukanda wa Pwani ya bahari wenye urefu wa kilometa 1,424 ambao ni muhimu kwa shughuli za uvuvi, ukuzaji viumbe maji na utalii.

Pia amesema ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania waweze kutumia nishati safi ya kupikia lengo ni kuhifadhi mazingira pamoja na kuboresha afya na ustawi wa jamii.