Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vipi kama ndoto ya Burundi kuungana na Tanzania ingetimia?

Muktasari:

Juzi, Julai mosi, wananchi wa Burundi waliadhimisha miaka 60 tangu nchi yao ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Jumapili ya Julai mosi, 1962. Mwaka moja kabla ya siku ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi wa Umoja Mataifa na chama kilichoshinda katika uchaguzi huo UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore, aliyemuoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili.

Juzi, Julai mosi, wananchi wa Burundi waliadhimisha miaka 60 tangu nchi yao ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Jumapili ya Julai mosi, 1962. Mwaka moja kabla ya siku ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi wa Umoja Mataifa na chama kilichoshinda katika uchaguzi huo UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore, aliyemuoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili.

Hata hivyo, Jumamosi ya Oktoba 13, 1962 Rwagasore aliyefikiriwa kuwa alikuwa anajenga uelewano wa kuishi pamoja kati ya Watutsi na Wahutu, aliuawa. Kifo chake kilikatisha ndoto ya shirikisho la Tanganyika na Burundi alilokuwa nalo Mwalimu Julius Nyerere.

Tanganyika ilipata uhuru Desemba 9, 1961 na baadaye ikawa Jamhuri Desemba 1962. Baada ya Uhuru wa Tanganyika katika hotuba yake kwa mkutano wa mwaka wa chama cha Tanu mwaka 1962, Mwalimu Nyerere alionyesha wazi kufadhaishwa kwake kulikotokana na mauaji ya Rwagasore.

Akizungumzia kundi jingine la wakimbizi, aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba nchi za Kiafrika zinafanya kila wawezalo kuwasaidia, lakini watu “wanatii amri kutoka kwa wageni ambao wanafaidika wakati Waafrika wanabeba mapanga dhidi ya Waafrika wenzao.”

Akiomboleza mauaji ya Prince Rwagasore nchini Burundi kama kikwazo dhidi ya maendeleo ya Taifa, alilinganisha mauaji hayo na yale ya Congo Kinshasa.

Aliuambia mkutano huo wa Tanu: “Hatupaswi kushangaa kama tutakuwa na Tshombe nyingine Ruanda-Urundi.”

Wakati huohuo, wafuasi wa Kitutsi wa mfalme wa zamani wa Rwanda walikusanyika kusini mwa Uganda na kuanza kufanya mashambulizi huku wakivuka mpaka. Serikali ya Gregoire Kayibanda aliyekuwa Rais wa Rwanda (Oktoba 1961 – Julai 1973) iliona uungwaji mkono wa Watutsi wa shirikisho kama mpango wa kurejesha “ufalme wa zamani wa Tanganyika-Rwanda-Burundi” na ikaishutumu Tanganyika kwa kuwahifadhi wanachama wa shirikisho hilo ambao walichukuliwa kuwa ni “shirika la kigaidi la Inyenzi.”

Wainyenzi walikuwa ni mkusanyiko wa Watutsi waliokuwa uhamishoni waliokuwa wakishirikiana na chama cha siasa cha Rwanda Union Nationale Rwandaise (UNAR), kilichokuwa kimeunga mkono utawala wa Kifalme wa Kitutsi ulioondolewa Rwanda.

Eneo lote la Tanganyika, Rwanda na Burundi lilijulikana kama Afrika Mashariki ya Kijerumani na Wajerumani waliliita ‘Deutsch-Ostafrika)’ kwa kifupi GEA.

GEA lilikuwa koloni la Kijerumani katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, ambalo lilijumuisha Burundi ya sasa, Rwanda, Tanzania Bara na Pembetatu ya Kionga, eneo dogo lililojumuishwa baadaye na Msumbiji.

Eneo la GEA lilikuwa na kilomita 994,996 za mraba (maili 384,170 za mraba). Hii ni kwa mujibu wa kitabu ‘History of East Africa’.

Eneo hilo lilikuwa karibu mara tatu ya eneo la Ujerumani ya sasa, na mara mbili ya eneo la mji mkuu wa Ujerumani wakati huo.

Ukoloni ulipangwa wakati jeshi la Ujerumani lilipoombwa mwishoni mwa miaka ya 1880 kukomesha uasi dhidi ya shughuli za Kampuni ya Afrika Mashariki ya Ujerumani. Hiyo ilimalizika baada ya Ujerumani kushindwa katika Vita vya Kwanza vya Dunia. Hatimaye, GEA iligawanywa kati ya Uingereza, Ubelgiji na Ureno na ikapangwa upya kama mamlaka ya Shirikisho la Mataifa (League of Nations).

Burundi ilipopata uhuru wake, umaarufu wa Rwagasore uliongezeka akawa kiongozi wa wanaharakati wa kupinga ukoloni. Alianzisha uhusiano na mzalendo wa Tanganyika Julius Nyerere, ambaye alimpatia ushauri na msaada wa kifedha.

Kwa mujibu wa kitabu ‘Building a Peaceful Nation Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania, 1960–1964’, uhusiano wa Rwagasore na Nyerere ulisababisha mshangao kwa utawala wa Ubelgiji, kiasi kwamba shirika la kijasusi la nchi hiyo lilianza kufuatilia hata mikutano yao na walifanya hivyo, angalau mara kumi kabla ya kifo cha Rwagasore.

Rwagasore aliungana na Nyerere katika kutetea uhuru, Uafrika na ujamaa. Hii iliwatia Wabelgiji wasiwasi. Walitishika zaidi wakati Rwagasore alipoongoza uanzishaji wa vyama vya ushirika, mfano wa ujamaa, na kutafuta uungwaji mkono na ufadhili kwa kutoka kwa viongozi wa kitaifa mahali pengine katika Afrika na Mashariki ya Kati.

Wabelgiji pia waliogopa uhusiano wa Rwagasore na mzalendo wa Congo, Patrice Lumumba, lakini Rwagasore na Lumumba hawakuwa karibu kama alivyokuwa karibu na Nyerere. Katika rekodi za kijasusi za Ubelgiji, Rwagasore na Lumumba walikutana mara mbili.

Kutokana na ukaribu ambao Nyerere na Rwagasore walikuwa nao, baadaye Nyerere alimbatiza mmoja wa wajukuu zake kwa jina la Louis kwa heshima ya Rwagasore. Mwaka 1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urundi uhuru kamili, lakini kila nchi pekee.

Kulingana na mchambuzi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Ezekiel Kamwaga, safari yake ya mwisho Rwagasore kutembelea Tanganyika ilikuwa ni mwanzoni mwa miaka ya 1960 na kumsimulia Mwalimu Nyerere ndoto yake moja kubwa; kwamba baada ya nchi zao kupata Uhuru, waunde Shirikisho la Tanganyika na Burundi. “Hiyo ndiyo kumbukumbu iliyobaki kichwani kwa Mwalimu wakati rafiki yake huyo akipanda ndege kurejea Bujumbura,” anaandika Kamwaga.

Kamwaga anasema Nyerere aliwasimulia kumbukumbu yake hiyo viongozi wa kisiasa wa taifa hilo mara kwa mara wakati akiwa msuluhishi wa mgogoro wa Burundi mwishoni mwa miaka ya 1990.

Kwa bahati mbaya, Rwagasore aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuwa Waziri Mkuu kwa wiki mbili tu. Kifo chake kinahusishwa na njama za wakoloni Wabelgiji pamoja na mivutano ya kikabila ya ndani ya Burundi.

Jumatatu ya Agosti 16, 1993, Mwalimu Nyerere alifanya mazungumzo na waandishi wa habari nyumbani kwake Msasani, Dar es Salaam, na kufafanua hotuba aliyoitoa kwa wabunge mwishoni mwa juma lililokuwa limepita kuhusu masuala mbalimbali ya Katiba ya Muungano. Katika mkutano huo aligusia suala la Burundi. Alisema:

“Kusema kweli kwanza Tanganyika ilikuwa inajumuisha Rwanda na Burundi. Hivi leo ingekuwa Wanyarwanda, Warundi tunao hapa pengine mngeamini kuwa Wanyarwanda na Warundi kiutamaduni wako karibu na Waswahili wa Tanga kuliko Waswahili wa Tanga walivyo karibu na Waswahili wa Pemba na Unguja! Pengine mngeamini.”

Vyovyote iwavyo, Tanzania, Rwanda na Burundi zingekuwa nchi moja kama zilivyokuwa wakati wa GEA, huenda hali ya kisiasa katika nchi hizo ingekuwa tofauti kabisa na ilivyo sasa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kamwaga zipo taarifa kwamba wazo la kurudi katika ndoto ya waasisi wa mataifa hayo zimeanza kusikika tena katika korido za Dodoma na Gitega. Je, marais Samia Suluhu Hassan na Evariste Ndayishimiye wanaweza kutimiza ndoto za Mwalimu Nyerere na Mwana wa Mfalme Rwagasore?