Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wabunge wa EU watoa tamko 'kutekwa' kwa Polepole


Muktasari:

  • Polepole aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ametekwa usiku wa kuamkia Oktoba 6, 2025 kwenye makazi yake Ununio, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya (EU), wameomba Serikali ya Tanzania kuchunguza aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole alipo.

Taarifa ya pamoja ya wabunge hao, imetolewa jana Oktoba 10, 2025 ikiwahusisha wabunge, Barry Andrews, Robert Biedrón, Udo Bullmann, Michael Gahler, Erik Marquardt na David McAllister.

“Tunaitaka Serikali ya Tanzania na mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kubaini alipo Polepole na kuhakikisha anarudi salama,” imeeleza taarifa hiyo.

Wametoa wito wa uchunguzi wa kina, huru na wa haki kuhusu madai yote ya matumizi mabaya ya polisi na matukio ya kupotea kwa watu.

Pia, wabunge hao wamesema kwa kuendana na (Falsafa ya 4R, Maridhiano, Mageuzi, Ustahimilivu na Kujenga upya) ya Rais Samia Suluhu Hassan kuanzishwe mazungumzo jumuishi ya vyama vyote vya siasa kuimarisha maridhiano na kuendeleza mageuzi ya kweli ya kisiasa nchini.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) pia kulaani tukio hilo na kuitaka Serikali kuchunguza kwa kina hali ya kutoweka kwa Polepole.

Kupitia taarifa iliyotolewa jana Oktoba 10, 2025 na Tume hiyo na kusainiwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Mathew Maimu amesema tukio linalodaiwa kutendwa na watu wasiojulikana limeketa taharuki kwenye jamii.

"THBUB inalaani na kukemea vikali vitendo hivyo kwani matukio kama haya ni uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wamisingi ya utawala bora ambayo yanahatarisha amani na utulivu wa nchi yetu"amesema Jaji huyo kupitia taarifa yake.

Polepole ajiuzulu nafasi yake ya ubalozi Julai 13, 2025 huku akitoa madai mbalimbali ambapo polisi imesema imefungua jalada la uchunguzi kuhusu madai hayo na kumtaka afike Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kutoa maelezo na ushahidi wa madai yake.

Polepole aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) anadaiwa kutekwa usiku wa kuamkia Oktoba 6, 2025 kwenye makazi yake ununio jijini Dar es Salaam.

Tayari Jeshi la Polisi, kupitia Msemaji wake David Misime, limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini ukweli wa kilichotokea.