Wabunge wataka mjadala wa elimu nchini

Tuesday May 04 2021
wabungepic

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo akiwasilisha bungeni maoni ya kamati hiyo kuhusu kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2021/2022, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

By Sharon Sauwa

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii nchini Tanzania imeitaka Serikali kuandaa  mjadala wa kitaifa wa elimu utakaowahusisha wadau mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Mei 4, 2021 na mwenyekiti wa kamati hiyo,  Stanslaus  Nyongo wakati akisoma maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2021/22.

Amesema  lengo la mjadala huo ni kupata suluhu ya kujua ni elimu ipi inafaa na kwa wakati gani.

Nyongo amesema Serikali ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga kwenye vyuo vingine vilivyo chini ya Baraza la Ufundi Nchini (Nacte).

“Wanafunzi hawa na ambao wengi wao wanatoka katika familia duni mara baada ya kuhitimu masomo yao ndiyo watakuwa watenda kazi hususan katika muktadha wa Tanzania ya viwanda,” amesema akibainisha kuwa hiyo itasaidia kuzalisha wataalamu wengi zaidi.


Advertisement
Advertisement