Wadau wa elimu watakiwa kuwekeza nguvu katika tafiti

Muktasari:

  •  Wadau wa elimu nchini wametakiwa kuwekeza nguvu katika kufanya tafiti zitakazowezesha kutatua changamoto katika jamii.

  

Arusha. Wadau wa elimu nchini wametakiwa kuwekeza nguvu katika kufanya tafiti zitakazowezesha kutatua changamoto katika jamii.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Dokta Mwamini Tulli katika kongamano la pili la uvumbuzi na ubunifu lililofanyika chuoni hapo.

Amesema ili Taifa liwe na jamii yenye maisha bora, inayopenda kujifunza, amani, utulivu na umoja, utawala na uongozi bora pamoja na uchumi wenye kuhimili ushindani lazima kuwe na tafiti zinazotoa dira na mwelekeo wa Taifa.

Amesema kuwepo kwa tafiti nzuri zilizofanywa na watalaamu zitasaidia kupata suluhisho la changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii.

Naye Mkuu wa Chuo cha IAA, Prof Eliamani Sedoyeka amesema kongamano hilo la pili lina lengo la kuwakutanisha pamoja wavumbuzi na wabunifu ili kujengeana uwezo ili ubunifu ulete tija.

Imeandikwa na

Happy Lazaro, mwananchi