Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wa haki za binadamu walaani ukatili mwanamke aliyeharibiwa mimba

Wadau wa haki za binadamu walaani ukatili mwanamke aliyeharibiwa mimba

Muktasari:

  • Wadau wa haki za binadamu nchini wamelaani tukio la kikatili lililofanywa na Mwenyekiti wa kijiji cha Samanga wilaya ya Moshi, Wilfredy Minja kwa kumrukisha kichura  zaidi ya saa mbili, Asha Rajabu(28) na kupelekea ujauzito wake wa miezi miwili alioutafuta kwa zaidi ya miaka mitano kuharibika.

Moshi.Wadau wa haki za binadamu nchini wamelaani tukio la kikatili lililofanywa na Mwenyekiti wa kijiji cha Samanga wilaya ya Moshi, Wilfredy Minja kwa kumrukisha kichura  zaidi ya saa mbili, Asha Rajabu(28) na kupelekea ujauzito wake wa miezi miwili alioutafuta kwa zaidi ya miaka mitano kuharibika.
Asha alifanyiwa ukatili huo ikiwa pamoja na kuchwapwa viboko Januari 24, mwaka huu kwa madai ya kuchelewa kufunga baa hadi saa sita usiku ambapo Februari 2 alipozidiwa na kukimbizwa hospitali ya Kilema iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
Wakizungumza na gazeti hili leo wadau wa haki za binadamu , wamesema tukio hilo ni la kinyama na halipaswi kufanywa na kiongozi wa serikali kwani kazi ya kiongozi ni kuhakikisha usalama wa wananchi wake huku wakiomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kali dhidi ya mwenyekiti huyo.
Anna Henga, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) amelaani tukio hilo na kusema kiongozi wa umma ana dhamana ya kuwalinda watu kwa mujibu wa katiba na sio kukiuka sheria na kujichukulia hatua mkononi.
“Hili tukio tunalilaani vikali, tena ni tukio la fedheha na halipaswi kufanywa na kiongozi kama huyo, huu ni ukatili ambao tumeendelea kuutolea matamko, huyu mwenyekiti achukuliwe hatua na ikiwezekana afukuzwe kazi kabisa lakini pia afunguliwe mashtaka ya shambulio la mwili na kuua,” amesema Anna
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika  lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kisheria na utetezi wa haki za binadamu (Ajiso),Virginia Silayo amesema tukio hilo ni la kidhalilishaji na ukatili kwa wanawake.
“Hebu fikiria binti anarukishwa kichura usiku wa manane kwa kosa tu la kuchelewa kufunga baa,amedhalilishwa na kupoteza ujauzito wake ambao ameusumbukia kwa miaka mingi,hili tukio sio la kufumbia macho jamii tunapaswa kulilaani vikali,na huyu aliyehusika na hili tukio achukuliwe hatua kali,” amesema Virginia.
Mpaka sasa  mwenyekiti huyo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo, ambapo Kaimu Kamanda wa polisi, Ronald Makona alisema atafikishwa mahakamani kwa kosa hilo  na wakati wowote atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.