Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wakutana Arusha kujadili masuala ya ushoroba

Arusha. Wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na sekta ya umma  wamekutana jijini Arusha kujadili biashara endelevu kwenye ushoroba wa kwa kuchinjwa unaounganisha njia kati ya hifadhi ya Tarangire na Manyara .

Akizungumza leo Machi 1, 2023  katika mkutano huo jijini hapa Meneja Miradi wa Taasisi ya TPSF, Max Rugaimukamu  amesema kuwa mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF)  kwa ufadhili wa USAID -Tuhifadhi maliasili Activity.


Amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuangalia namna ya kufanya biashara yenye uendelevu zinazojali na kuangalia mazingira ya wanyamapori pamoja na kujadili changamoto na mapendekezo ya kikodi  na zisizo za kikodi sambamba na kuzungumzia  maboresho katika maeneo  hayo ili kuwekeza uwekezaji na biashara  katika sekta ya utalii na mifugo.

Ameongeza kuwa taasisi  hiyo imekuwa ikifanya kazi katika kuleta ufahamu kwa sekta binafsi juu ya umuhimu wa ushoroba katika uhifadhi wa maliasili na ukuzaji wa uchumi .

"Unajua tunawapa mafunzo ili waweze kujua umuhimu wa kutunza ushoroba kwani endapo zitatunzwa inasaidia pia kutunza misitu, wanyamapori na vitu vyote vilivyopo ndani ya ushoroba "amesema

Kwa upande wake Meneja  ushirikishwaji wa sekta binafsi kutoka shirika la RTI International wasimamizi wa mradi wa USAID Tuhifadhi maliasili, Dkt Elikana Kaluwanga amesema mradi huo unatekelezwa maeneo mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuwepo kwa usimamizi mzuri wa shoroba (mapito ya wanyamapori).

Amesema wadau hao wa sekta ya utalii kutoka sekta binafsi na umma kwa pamoja wameweza kujadili fursa za utalii na ufugaji  zilizopo katika maeneo ya ushoroba na kupata mafunzo namna ya kuweza kuendelea kutunza shoroba hizo ili ziendelee kuwepo na kutumiwa  na wanyamapori kwa ajili ya kuongeza utalii zaidi .


"Mradi huu unalenga kuwezesha wadau hao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika usimamizi wa maliasili hasa shoroba kwani kwao  ni muhimu sana kama wawekezaji wakubwa katika sekta ya utalii."amesema.

Ameongeza, sasa hivi serikali ya Tanzania imefikia hatua ya kuyaainisha hayo maeneo  ili yasipotee ambapo kwa Tanzania kuna takribani shoroba 61 hivyo ni jukumu lao  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na wananchi kuhakikisha wanaunga  mkono  na kutoa kipaumbele kwenye masuala ya shoroba, huku akiomba serikali kuweka alama ili kunusuru kizazi hiki na kijacho.

Naye Mmoja wa wadau wa utalii, Mkurugenzi  wa Jumuiko la Maliasili Tanzania, Zakaria Faustin amesema kuwa,ni vizuri serikali ikafanya  mabadiliko ya huo mwongozo wa maeneo ya mapito ya wanyama  ili kuainisha matumizi mbalimbali na wananchi wawe na imani kuwa maeneo hayo hayachukuliwa na serikali bali yataendelea kuwa  ya kwao.