Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima kuboreshewa mawasiliano kidigitali kwa simu janja

Dodoma. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hasa katika huduma ya mawasiliano kampuni ya Yas, imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuleta mabadiliko ya kidigitali kwa wakulima kwa kuendeleza mpango wa ‘Device Financing’, unaowawezesha wakulima kumiliki simu janja kwa gharama nafuu kupitia malipo ya awamu.

Kupitia mpango huo mkulima anaweza kuanza kutumia simu janja kwa kulipa kuanzia shilingi 1,400 kwa siku kwa kipindi cha miezi sita.

Akizungumza katika maonesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma, Meneja wa Yas Kanda ya Kati, Frank Anthony, amesema mpango huo umetengenezwa mahsusi kwa ajili ya wakulima wa vijijini na wenye kipato cha chini, ambao wanahitaji teknolojia ili kuimarisha shughuli zao za kilimo lakini wanakumbwa na changamoto ya gharama za vifaa.

“Katika ulimwengu wa leo wa kidigitali, simu janja si kifaa cha anasa, ni nyenzo muhimu inayowawezesha wakulima kupata taarifa za hali ya hewa, bei za mazao, masoko, na elimu ya kilimo kwa njia ya mtandao,” amesema Frank Anthony.

Simu zinazotolewa kupitia mpango huo zinakuja tayari zikiwa zimeunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi na huduma za kifedha kupitia mtandao huo.

Kwa njia hiyo, wakulima wanaweza kufanya miamala ya kifedha, kushiriki kwenye vikundi vya mafunzo ya kilimo mtandaoni, na kutumia fursa nyingine nyingi za kidigitali kuboresha maisha yao na shughuli zao.

“Mpango huu unawasaidia wakulima kuwa sehemu ya mapinduzi ya kidigitali, kutoka kuuza mazao hadi kupata elimu ya mbegu bora na mbinu za kisasa za kilimo,”ameeleza na kuongeza:

” Tunapunguza pengo la kidigitali na kuhakikisha kila mkulima anapata fursa sawa ya kujifunza, kuwasiliana na kujiendeleza,”