Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima kupewa mbinu kilimo biashara

Mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa huru la Kilimo (Ansaf), Honest Mseri akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa kimataifa wa kilimo leo Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Licha ya asilimia 65 ya Watanzania kujiajiri kwenye kilimo, bado wanakosa mbinu za kibiashara hali ionayoendeleza umasikini wa kipato na pato la Taifa.

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji (NEEC), Bengi Mazana Issa amesema kuna haja ya kuwaongezea ujuzi wakulima nchini ili waondokane na kilimo cha mazoea na kukifanya kuwa kilimo biashara.

Mazana  amesema hayo leo Julai 10, 2024 alipokuwa akizindua mtandao wa kimataifa wa kilimo biashara (AMEA) unaounganisha zaidi ya nchi 80 duniani kwa kutoa utaalamu wa kilimo biashara kwa wakulima wadogo.

Amesema licha ya Watanzania wengi kujiajiri katika kilimo, bado wengi hawana ujuzi wa biashara na hivyo kuishia kuwa masikini.

 “Takwimu ziaonyesha eneo la uingizwaji biashara katika kilimo linachangia pato la Taifa chini ya asilimia 2 na hii yote ni kwa sababu Watanzania hawana ufahamu wa utaalamu wa biashara,” amesema.

Amesema bazara la uwezeshaji kiuchumi linashirikiana na AMEA kama mkono wa Serikali kuhakikisha wakulima wanafikiwa na kupewa mbinu.

“Tunajua kwamba Watanzania wengi wamejiajiri kwenye kilimo, kwa hiyo kama kilimo kitafanywa kwa tija tunaweza kufanya vizuri na kuchangia kwenye pato la Taifa.  

 “Mtandao huu wa AMEA utatuunganisha na mataifa mengine kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kufaidika na huduma za ushauri wa kibiashara hivyo wakulima wetu wafanye kilimo cha biashara,” amesema.

Mkurugenzi wa AMEA duniani, Mark Blackett akieleza jinsi mtandao huo unavyofanya kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa huru la Kilimo (Ansaf), Honest Mseri amesema njia bora ya kuwapa mbinu wakulima kuhusu kilimo biashara ni kuimarisha vyama vya ushirika.

“Tumekuwa tukijiuliza tufanyeje ushirika uweze kukopesha wakulima? Tunafanyaje kufikia masoko? Kwa hiyo ujio wa AMEA utasaidia vyama vya ushirika kuwasaidia wakulima.

“Ili mkulima ajiunge na chama cha ushirika lazima aone tija, vinapoleta faida zaidi ndipo wakulima watahamasika kujiunga zaidi,” amesema.

Amesema lengo la kuingia kwenye AMEA ni kusaidia kilimo biashara kiwainue wakulima kiuchumi.

“Kwa sasa kuna mazao ya mbogamboga na matunda yanayopelekwa kwa wingi nje ya nchi, lakini kinachoangaliwa ni ubora, kwa hiyo tunatakiwa kuangalia huo ubora kwa wakulima ili waweze kuuza mazao nje ya nchi.

“Kwa mfano tumeona zao la korosho linaendelea kuongezeka nje ya nchi, hivyo ubora katika uzalishaji unapaswa kuzingatiwa,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa AMEA duniani, Mark Blackett amesema mtandao huo upo kwa ajili ya kusaidia mitandao ya wakulima na kutoa mbinu za kilimo.

“Matokeo katika mitandao tuliyonayo yameonyesha kuboreka kwa uzalishaji wa kilimo na biashara. Tunahitaji kuwaleta kwa pamoja wadau wanaounga mkono kilimo vikiwamo vyama vya ushirika na asasi za kiraia na Serikali ili kusaidia kupatikana kwa mbinu zitakazowezesha biashara ya kilimo na kuacha kupoteza muda kwenye mambo ambayo hayaleti tija kwa wakulima,” amesema.