Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima waomba mbegu bora kufungua soko la mchele kimataifa

Morogoro. Wakati Serikali ikiendelea kuimarisha na kuongeza maeneo ya umwagiliaji, wakulima wa mpunga nchini wameiomba kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora kwa gharama nafuu ili kuongeza tija na kuwezesha mchele wa Tanzania kuingia kwenye soko la kimataifa kwa ushindani.

Wameeleza kuwa bila kuimarishwa kwa vyanzo vya uhakika vya mbegu zenye kustahimili magonjwa na mabadiliko ya tabianchi, uzalishaji unaendelea kuwa wa chini na mchele wa ndani unakosa mvuto sokoni.

“Tunazalisha kwa gharama kubwa, lakini mchele wetu hauna ushindani sokoni. Tunahitaji mbegu bora kwa bei nafuu ili nao mchele wetu uweze kushindana kimataifa,” amesema Natoto Omary, mkulima kutoka Wilaya ya Mvomero, katika mkutano wa wadau wa mbegu, umwagiliaji na biashara ya mpunga uliofanyika mjini Morogoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mchele Tanzania, Geoffrey Rwiza amesema licha ya juhudi za tafiti zinazofanyika, bado kuna changamoto katika upatikanaji wa takwimu sahihi za uzalishaji na sheria za kusimamia ubora wa mchele, hali inayokwamisha mikakati ya kuuza nje.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Ushirika na Umwagiliaji, Dk Stephen Nindi amesema Serikali imeanzisha zaidi ya miradi 700 ya umwagiliaji na inaendelea kuimarisha taasisi za uzalishaji na udhibiti wa mbegu bora ili kuhakikisha wakulima wanapata mbegu zenye ubora kwa bei nafuu kupitia ruzuku.

“Katika mwaka wa fedha 2025/26 moja ya sekta ambazo zinaenda kuimarishwa ni pamoja na sekta ya upatikanaji wa mbegu bora, tunaimarisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) ili tuweze kuzalisha mbegu za msingi, tunaimarisha taasisi yetu inayohusika na uzalishaji wa mbegu (ASA) lakini pia tunaenda kusimamia usambazaji wa mbegu bora kwa wakulima wetu hapa nchini,” amesema Dk Nindi.