Waliokufa Ziwa Victoria wafikia 12

Muktasari:

Watu waliookolewa wakiwa hai katika ajali hiyo ni watatu.

Idadi ya watu waliokufa baada ya Toyota Hiace kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 12.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu amesema katika ajali hiyo watu watatu wameokolewa wakiwa hai.

Msangi amesema walionusurika wameokolewa na wananchi ambao ni wataalamu wa kuogelea.