Wana CCM 19 wajitokeza kumrithi Kwandikwa Ushetu

Wednesday September 01 2021
Kwandikwa pc
By Shaban Njia

Kahama. Wakati uchukuaji wa fomu wa kuwania ubunge katika jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga ukikamilishwa, wanachama 19 wa CCM wamejitokeza, wanaume wakiwa 17 na wanawake wawili.


Uchaguzi wa jimbo hilo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa aliyefariki dunia Agosti 2, 2021 jijini Dar es Salaam.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Septemba 1, Mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM, Emmanuel Mbamange amesema, wanachama wote waliochukua fomu wamerejesha kwa wakati na hakuna fomu iliyoharibika.


Amewataka wagombea hao kuwa ni  Samson Lutonja, Makoye Mayengo, James Lembeli, Bundala Shija, Paschal Michael, Emmanuel Charahani, Yohana Masonda, Ernest Nila, Ahmed Haroun, Betha Juma, Mhandisi Manyango Nchambi, Marry Lema, Erhard Mlyasi na Dk Mathew Masele.

Soma hapa:CCM yafungua pazia la wagombea jimbo la Ushetu

Wengine ni pamoja na Dk Lameck Makoye Nyaligwa, Marthin Mwakatundu, Makwaya Michael, Jorodani Balindo pamoja na Profesa Simon Julius Maziku.

Advertisement


Hata hivyo, Mbamange amesema kazi inayofuata ni upigaji wa kura za maoni utakaoshirikisha wajumbe halali wa chama hicho 880 na kwamba mgombea atakayeshinda atakuwa bado hajateuliwa mpaka atakapothibitishwa.


Amesema jimbo hilo linawapiga kura 165,418 na kuwasisitiza wagombea kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Soma hapa: Lembeli autaka ubunge jimbo la Ushetu

Kwa upande wake katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Donald Magessa amesema kuwa, maandalizi ya kupiga kura za maoni kwa watia nia yamekamilika na uchaguzi huo utafanyikia katika ukumbi wa sekondari Dakama wilayani humo.

Advertisement