Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi Maswa waomba ushirikiano utunzaji mazingira

Takataka ambazo hazijaondolewa katika eneo la Sola Ginner mjini Maswa. Picha na Samwel Mwanga

Muktasari:

  • Taka nyingi huonekana kutupwa ovyo katika maeneo mbalimbali, jambo linaloweza kuhatarisha afya za wakazi iwapo halitapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Maswa. Wananchi wa mji wa Maswa mkoani Simiyu wametoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kutunza usafi wa mazingira kufuatia kuongezeka kwa taka katika baadhi ya maeneo.

Wamesema licha ya jitihada za Mamlaka ya Mji Mdogo wa Maswa na mzabuni wa ukusanyaji taka, huduma hiyo bado haijafika ipasavyo hasa maeneo ya pembezoni, hali inayosababisha taka kukaa muda mrefu na kuhatarisha afya.

Mkazi wa Sola, Paul Shija amesema huduma inaonekana zaidi katikati ya mji, huku pembezoni kukiwa na changamoto. Naye Rehema Alexander wa Biafra A amesema baadhi ya wananchi hawazingatii usafi, wakitupa taka ovyo.

Viroba vilivyo na takataka ambavyo vinasubiri kuondolewa katika mtaa wa Unyanyembe mjini Maswa. Picha na Samwel Mwanga

Mfanyabiashara wa Soko la Maswa, Jasmin Halfan ameonya kuwa ucheleweshaji wa uondoaji taka unaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Maswa, Caroline Shayo amesema wanafahamu changamoto hizo na wanaendelea kufanya tathmini kuboresha huduma huku wakitoa elimu kwa wananchi kushiriki katika kudumisha usafi