Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi waeleza wanavyotumia bodaboda kupeleka mahindi Kenya

Vijana wa bodaboda wakiwa wamepakia magunia ya mahindi kwenye pikipiki wakivusha kwa njia za panya kupeleke nchini Kenya. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

 licha ya nchi ya kenya kupiga marufuku mahindi ya tanzania kuingia nchini humo kwa madai ya kuwa na sumu kuvu, baadhi ya wananchi wanatumia bodaboda kuvusha mahindi hayo kwa kutumia njia za panya.

Rombo. Licha ya nchi ya Kenya kupiga marufuku mahindi ya Tanzania kuingia nchini humo kwa madai ya kuwa na sumu kuvu, baadhi ya wananchi wanatumia bodaboda kuvusha mahindi hayo kwa kutumia njia za panya.


Mahindi hayo ambayo hupakiwa kwenye bodaboda zaidi ya magunia matatu hupelekwa nchini Kenya kwa kutumia njia hizo hadi eneo la Taveta ambalo inadaiwa hupakiwa kwenye magari yao.


Mwananchi Digital leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 limefika mpaka wa Holili na kushuhudia pikipiki zaidi ya 50 nyingine zikitokea Kenya zikiwa zimepakia magunia ya mahindi.


Emmanuel Sauli ,dereva bodaboda amesema  wanatumia njia za panya  kuvusha mahindi hayo na hulipwa Sh2,000 kwa gunia moja.


"Tunaamka usiku kuvusha  mahindi kwa njia za panya kupeleka mpaka nchi ya Kenya eneo la Taveta na kila gunia moja tunalipwa Sh2,000, tukifika tunakabidhi mizigo yao na wanapakia kwenye magari yao," amesema Sauli.


Dereva mwingine wa bodaboda, Evans Christipine amesema mara nyingi wamekuwa wakisafirisha mahindi kwa njia za panya baada ya nchi ya Kenya kuweka zuio la mahindi kuingia nchini humo.


"Baada ya Kenya kuweka zuio la mahindi ya Tanzania kutoingia nchini Kenya kwa kweli tulitaabika sana, kwa hiyo tulipopata fursa hii ya kupitia njia za panya kupeleka mahindi imetusaidia sana maana hali ilikuwa mbaya ya kipato na hii kazi ndio tulikuwa tukiitegemea, kwa siku naweza kupeleka mahindi na pikipiki zaidi ya mara 15,"amesema.