Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi washauriwa kuhama maeneo yaliyopasuka Same

Muktasari:

  • Wananchi wa Marieni wamehama makazi kutokana na ardhi kupasuka na kutitia, wakikabiliwa na hifadhi duni. Wataalamu wanasisitiza tahadhari hadi uchunguzi wa kina utakapobaini chanzo cha hali hiyo.

Same. Mtaalamu wa jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania, Gabriel Mbogoni, amewashauri wananchi wa Kijiji cha Marieni, Kata ya Chome, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, kuchukua tahadhari ikiwamo kuondoka katika maeneo yao.

Ushauri huo umetolewa kufuatia hali ya ardhi katika eneo hilo kuendelea kutitia na kupasuka, jambo linalohatarisha usalama wa wananchi.

Mpaka sasa, zaidi ya kaya 10 katika vitongoji vya Makandeni, Kungwini na Marieni zimeyahama makazi yao kutokana na hofu iliyosababishwa na nyufa hizo.

Hali hiyo pia imeathiri shughuli za kijamii, ambapo baadhi ya waumini wa Kanisa la Wasabato Kungwini wamekosa mahali pa kuabudia baada ya maeneo yao kuharibiwa.

Kufuatia changamoto hiyo, baadhi ya wananchi walioathirika wamehamisha familia zao pamoja na mali zao na kuelekea katika maeneo ya hifadhi ya muda wakisubiri hatua zaidi kutoka Serikalini.

Baadhi ya wananchi wakionyesha eneo karibu na kanisa la Wasabato Kungwini ambalo limepata mpasuko mkubwa kutokana na baadhi ya vipande vya aradhi kupishana.

Wananchi hao, ambao wameyahama makazi yao kwa zaidi ya wiki mbili sasa, wameendelea kuiomba Serikali kuwasaidia kupata suluhisho la kudumu.

Wamesema hifadhi wanazoishi kwa sasa ni za muda na zinakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo watoto kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kijamii kama shule baada ya kuhama makazi yao ya awali.

Aprili Mosi, 2026, Mwananchi lilifika katika eneo hilo na kushuhudia moja ya kanisa  likiwa limeachwa wazi baada ya kuta zake kupasuka kwa nyufa kubwa, sakafu yake ikionyesha dalili za kutitia huku makazi ya wananchi hao waliyoaacha yakiwa tupu.

Moja ya eneo la kanisa la Wasabato, ambalo lipo katika Kitongoji cha Makandeni, Kijiji cha Marieni, ambalo limeachana   kutokana na ufa mkubwa ambao umepita katika eneo hilo la kanisa.

Hata hivyo, mwaka 2009 katika Kitongoji cha Manja, kata ya Mamba Myamba wilayani humo, watu 24 walifariki dunia baada ya kuangukiwa na maporomoko ya udongo na magema, hali ambayo ilipelekea baadhi ya maeneo ya wananchi hao kuhama katika maeneo hayo.

Akizungumza leo Aprili 3, 2026 na gazeti hili mtaalamu huyo, amesema tahadhari ya wananchi kuondoka katika eneo hilo ni muhimu hadi pale eneo hilo litakapofanyiwa utafiti wa kina ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.

Aidha, Mbogoni amesema mpasuko wa ardhi unaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, ikiwemo matetemeko ya ardhi, uwepo wa nyufa chini ya ardhi, au ardhi kukosa uimara wa kushikilia tabaka zake kutokana na mabadiliko ya kijiolojia.

"Kuna vitu vingi ambavyo vinapelekea mpasuko wa ardhi, inaweza ikawa ni tetemeko la ardhi, kutitia tuu kwa ardhi kwamba chini kuna mpasuko kwasababu ukanda wa Same upo kwenye eneo la bonde la ufa,"amesema Mbogoni

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Marieni, kata ya Chome, akionyesha moja ya eneo ambalo limeathiriwa na mpasuko wa ardhi ambao umepelekea baadhi ya maeneo kutitia.

Mbogoni amesema kwa sababu bado eneo hilo halijapimwa na kujua chanzo cha hali hiyo ni nini ni vyema wananchi hao wakaondoka maeneo hayo kwa usalama wao mpaka hapo wataalamu watakapochunguza chanzo cha hali hiyo.

"Kwa sababu haijulikani ni kitu gani ni vizuri wananchi wakaondoka katika hayo maeneo kama walivyofanya mpaka pale tutakapowaambia hicho ni kitu gani ambacho kimetokea kwasababu hiyo hali bado inaonekana inaendelea," amesema Mbogoni. 

Amesema; "Hiyo ndio njia ya tahadhari kwa sasa, mpaka pale wataalamu watakapofika waseme ni kitu gani, vinginevyo waondoke katika maeneo hayo hatari kwasababu nimeona mipasuko ni mikubwa, ni vyema waondoke

Hata hivyo,  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kutokana na changamoto hiyo, tayari Serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kwa kuagiza wataalamu kwenda eneo hilo kufanya uchunguzi wa kina katika maeneo hayo.

“Nimeshapokea taarifa na nimeshaelekeza wataalamu waende haraka ili kubaini chanzo cha tatizo na hatua stahiki za kuchukua,” alisema RC Babu.


Waomba wataalamu


Akizungumza mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Elisa Mtera, ameiomba Serikali kupeleka wataalam katika eneo hilo ili chunguza tatizo hilo linasababishwa na nini.

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Marieni, kata ya Chome, akionyesha moja ya eneo ambalo limeathiriwa na mpasuko wa ardhi ambao umepelekea baadhi ya maeneo kutitia.

"Tunaomba Serikali ituletee wataalamu, waje waangalie ni kitu gani hiki, maana kadri siku zinavyozidi kwenda mipasuko inaongezeka na sisi inatutia hofu zaidi, kwa sababu hatujui ni kitu gani kipo chini ya ardhi," amesema mwananchi huyo.

Anna Mndeme, mmoja wa waathirika wa tukio hilo, amesema kutokana na changamoto hiyo amelazimika kuyakimbia makazi yake kutokana na makazi yao kuathiriwa na mpasuko wa nyufa hali ambayo inawapa hofu kubwa na kutishia usalama wao.

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Marieni, kata ya Chome, akionyesha moja ya eneo ambalo limeathiriwa na mpasuko wa ardhi ambao umepelekea baadhi ya maeneo kutitia.

"Hapa nilipo nipo kwa ndugu zangu wamenipa hifadhi ya muda  baada ya kuondoka nilikokuwa naishi, nyufa zimekuwa ni kubwa na zimepasua nyumba yangu na hata eneo la nyumba yangu kuna mipasuko mikubwa na kila siku inaongezeka, hivyo tunaomba Serikali itume wataalam wake wake hapa, kabla maafa makubwa hayajatokea," amesema.