Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanandoa wanaodaiwa kusafirisha dawa za kulevya wasota rumande

Mshtakiwa Najim Mohamed, anayekabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 3,050 akiwa chini wa ulinzi wa askari Magereza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Maktaba

Muktasari:

 Washtakiwa wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya Desemba 15, 2023 eneo la Kibugumo Shule, Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam. Serikali imesema bado inaendelea na upelelelezi katika kesi ya kusafirisha kilo 3,050 za dawa za kulevya inayowakabili watu watatu akiwamo mtu na mke wake.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 53/2023 ni Najim Abdallah Mohamed (52), mke wake, Maryam Najim Mohamedi (50) na mfanyakazi wa ndani wa kiume, Juma Mbwana Abbas (37).

Leo, Januari 11, 2024, Wakili wa Serikali, Frank Michael amedai kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado unaendelea, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Michael ametoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aaron Lyamuya.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Lyamuya ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 27, 2024 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili kuwa hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo, Desemba 29, 2023 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka mawili.

Wakili Halfan amedai kuwa,  Desemba 15, 2023 katika eneo la Kibugumo Shule lililopo Kigamboni,  washtakiwa kwa pamoja walidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilo 882.71.

Katika shtaka la pili, siku na eneo hilohilo, washtakiwa wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye uzito wa kilo 2,167.29.