Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapatiwa msaada wa kisheria watolewa bure Manyara

Mkurugenzi wa Programu na Uendeshaji kutoka Legal Services Facility (LSF), Amani Manyelezi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Mama Samia Mkoani Manyara.

Muktasari:

  • Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imelenga kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini na itadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Manyara. Wasaidizi wa msaada wa kisheria kutoka wilaya zote mkoani Manyara wameshiriki katika uzinduzi wa kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Kisheria mkoani hapa na kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi bure.

 Malengo ya kampeni hiyo inayofadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF) ni pamoja na kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususani haki za wanawake na watoto, kuimarisha huduma ya ushauri wa kisheria na kutatua migogoro kwa wananchi na kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa huduma za kisheria na kufanya huduma hizi kuwa endelevu.

Akizungumza leo Mei 24 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo mkoani hapa, Mkurugenzi wa Programu na Uendeshaji kutoka LSF, Amani Manyelezi amesema,

“Kampeni hii imekwenda sambamba na kazi tunazozifanya kwa takribani miaka 11 za kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wote kupitia watoa huduma zaidi ya 4,000 waliopewa mafunzo ya kisheria nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar.”

Manyelezi amesema kwa mwaka wanawafikia watu milioni saba kupitia elimu ya kisheria. 

“Vilevile tunapokea migogoro takribani 70,000 ambapo asilimia 60 inatatuliwa na wasaidizi wa kisheria na hivyo kupunguza msongamano mahakamani.” 

Katika utekelezaji wa kampeni hiyo, huduma za msaada wakisheria zimetolewa katika viwanja vya Stendi ya zamani Manyara na itaendelea katika muda wa siku 10 mfululizo kwa wilaya zote za mkoa wa Manyara ikiwemo Babati, Hanang, Simanjiro, Mbulu TC, Mbulu DC na Kiteto, ambapo katika siku pekee ya ufunguzi wasaidizi wa kisheria wamepokea kesi 45 na kuzishughulikia.