Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano wadakwa na ETS feki Same

Muktasari:

  • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kufanya msako wa wafanyabiashara wasiowaaminifu ambao wanatumia stempa feki za kielektroniki kwa lengo la kutengeneza faida kubwa na kuikosesha mapato Serikali.

Same. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kilimanjaro imesema imewabaini wafanyabiashara watano waliokuwa wakitumia stempu feki za kielektroniki (ETS) zenye nembo ya TRA kwenye vinywaji.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Jauari 27, 2021 na Ofisa msimamizi wa kodi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Odupai Papaa.

Alikuwa akizungumza na wafanyabiashara kwenye hitimisho la siku ya utoaji elimu kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Same, ili mbalimbali zinazowakabili katika kazi yao.

“Kuna baadhi ya wafanyabiashara tumewabaini wanamiliki stempu feki za kielektroniki wanazobandika kwenye vinywaji, hapa Same tumewabaini watano tayari na tumewabaini baada ya kuendesha hili zoezi hapa Mkoani Kilimanjaro. Nasema  wale wote ambao tumewabaini, hatua stahiki za ukwepaji kodi zitachukuliwa dhidi yao,” amesema Papaa.

Aidha, amesema kuna vifaa maalumu vinavyotumiwa na TRA hivi sasa kutambua mchezo huo mchafu unaofanywa na baadhi  ya wafanyabiashara wakubwa ambao si waaminifu wakilenga kukwepa kutoa mapato ya Serikali.

“Kwa kutumia vifaa vyetu maalumu tulivyonavyo, ukimulika nembo ya TRA iliyopo kwenye hivyo vinywaji inagundulika kuwa ni feki au sio feki, kwa hiyo tutawakamata wote, la sivyo waache kufanya mchezo huo,” amesema.

“Hawa watano tuliowakamata hapa Same tutawachukulia hatua za kisheria kwa sababu wamedhamiria kuikosesha serikali yetu mapato,” amesema Papaa.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara wanasema baadhi yao wanajaribu kutafuta njia ya mkato kupata faida, kutokana na ugumu wa biashara uliopo sasa.

"Watu wanafanya mbinu mbalimbali ili tu kuhakikisha biashara zao hazikwami, ndiyo  maana wanaamua kupita njia zisizo halali kama hiyo ya kutengeneza stempu feki,” anasema Eliasante Ngolo.

Amesema kama TRA itaendelea kutoa elimu kwao ya nini wakifanye, huenda wengi wakaelimika na watafanya biashara halali.