Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu wafariki gari dogo likigongana na lori

Muktasari:

Chanzo cha ajali hiyo ni kimeelezwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya Toyota Hillux aliyehama upande wake wa kushoto bila kuchukua tahadhari.

Lindi. Watu watatu wamefariki dunia baada ya gari walilopanda kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Mipingo barabara ya Lindi – Nangurukuru mkoani hapa.

 
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi January 20, 2024 kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Makuri amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2 usiku katika eneo la Mipingo.

Kamanda Makuri amefafanua kuwa gari lenye namba za usajili T265DWP aina ya FAW lilikuwa linatokea Dar es Salaam kwenda mkoani Lindi, ambapo dereva wa lori hilo amegongana uso kwa uso na gari la Halmashauri ya Kilwa aina ya Toyota Hillux lenye namba za usajili SM14438 lililokuwa linatokea mkoani Lindi kuelekea kijiji cha Kilanjelanje Wilayani Kilwa.

Kamanda Makuri amewatataja waliofariki kuwa ni dereva wa gari la Halmashauri ya Kilwa, Ally Mwaliba (30), Tumain Mbando (33) mfanyakazi Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Lindi pamoja na Farida Maulanga (20) mkazi wa Masasi mkoani Mtwara.

"Huyu dereva wa gari la Halmashauri ya Kilwa, alihama upande wake wa kushoto na alipokuwa anarudi upande wa kulia ndipo akakutana na lori na kusababisha wote waliopo kwenye gari hilo kufariki," amesema Kamanda Makuri.

Amesema kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika hosptali ya Sokoine mkoani Lindi.

Pia ameongeza kuwa wanamshikilia George Tibu (28) dereva wa lori na mkazi wa Jijini Dodoma

"Nitoe wito kwa madereva kuwa makini wanapokuwa barabani,ili kuepuka ajali ambazo zinakatisha maisha ya watu" amesema pia