Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

Muktasari:

Kaimu kamanda Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Morogoro, Emmanuel Ochieng amesema mpka sasa wameokoa watu 48 waliokuwa wamezingirwa na maji katika maeneo ya kata ya Kihonda kufuatia mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia leo Ijumaa Januari 13, 2023.



Morogoro. Kaimu kamanda Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Morogoro, Emmanuel Ochieng amesema mpka sasa wameokoa watu 48 waliokuwa wamezingirwa na maji katika maeneo ya kata ya Kihonda kufuatia mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia leo Ijumaa Januari 13, 2023.

Ochieng Amesema watu hao kwa Sasa wamehifadhiwa ofisi ya kata ya Kwa ajili ya kupatiwa msaada wa chakula,malazi na mahitaji mengine.

Aidha amesema wananchi wakatakiwa kuchukua tahadhali kutokana na mvua hizo huku akiwataka wale waliochimba mashimo ya choo, takataka kuhakikisha wanayafukia ili yasiweze kuleta athari zaidi.

Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro