Watumishi 23 Moi wachunguzwa madai ya wizi wa dawa, vifaa tiba

New Content Item (1)
Watumishi 23 Moi wachunguzwa madai ya wizi wa dawa, vifaa tiba

Muktasari:

Watumishi 23 wa Idara  ya  Famasia katika Taasisi ya Mifupa (Moi) wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya wizi wa dawa  na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh1.2 bilioni.

Dar es Salaam. Watumishi 23 wa Idara  ya  Famasia katika Taasisi ya Mifupa (Moi) wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya wizi wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh1.2 bilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Januari 13, 2021 na  mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Mbungo amesema watumishi hao wanadaiwa kufanya udanganyifu huo kati ya mwaka 2018 hadi 2020.

Akielezea namna ubadhirifu huo ulivyofanyika, Mbungo amesema, watuhumiwa hao walikuwa wanaandika taarifa za uongo katika mfumo unaofahamika kama MEDPRO4 kwa kuweka idadi kubwa ya vifaa vilivyotolewa tofauti na idadi halisi iliyotolewa na madaktari kwa wagonjwa na wateja.