Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wafa maji wakivua samaki Ziwa Victoria

Muktasari:

  • Upepo mkali unaovuma Ziwa Victoria umesababisha dhoruba hivyo watu wawili kupoteza maisha wakati wakivua.


Buchosa. Watu wawili wakazi wa Kijiji cha Busikimbi, Kata ya Maisome, Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza waliokuwa wakivua samaki ndani ya Ziwa Victoria wamepoteza maisha baada ya chombo walichokuwa wakitumia kuvulia samaki  kukumbwa na dhoruba kisha  kupinduka na  kuzama.

Kaimu Ofisa Mtendaji, Kata ya Maisome, Revocatu Mchele amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea usiku wa kuamika Juni 8 mwaka 2022 saa tano usiku na kuwataja waliopoteza maisha kuwa Baraka Kazimili (24) pamoja na Shadrack Mbonabucha (22) wote wakazi wa Kijiji cha Busikimbi, Kata ya Maisome.

Amesema  upepo mkali unaovuma ndani ya Ziwa Victoria kwa sasa unaweza kuleta madhara kwa wavuvi kama hawatachukuwa tahadhari  zinatolewa na mamlaka ya hari ya hewa Tanzania juu ya uwepo wa kipindi cha upepo mkali  utakaodumu hadi mwezi Agosti mwaka huu.

Mchele amesema hadi sasa miili ya watu hao haijapatikana na jitiahada za wananchi zinaendelea kuwatafuta.

Mmoja wa wakazi wa Kata ya Maisome,  Tulubuza Galubundu amesema matukio haya ya watu kupoteza maisha wakivua samaki ndani ya ziwa kipindi cha kiangazi hutokea mara kwa mara hivyo elimu  inatakiwa kutolewa kwa wavuvi ili kujikinga na hali hiyo.

Mkuu wa Wilaya Sengerema Senyi Ngaga amesema amepata taarifa juu ya tukio hilo na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linakwenda Kijiji cha Busikimbi, Kata ya Maisome kutafuta miili hiyo.

Ngaga ametoa rai kwa jamii ya wavuvi na watu wanaotumia mitumbwi kusafirisha abiria ndani ya Ziwa Victoria kuchukua tadhari wanapofanya shughuli zao ndani ya Ziwa Victoria.