Waziri ataja umuhimu sera uchumi wa buluu
Waziri wa Utalii na mambo ya kale Simai Mohamed Said akiwa amesimama nyuma ya mtoto, huku akionekana mwenye nyuso ya furaha baada ya kuzindua Crowne hotel Plaza
Muktasari:
Waziri wa Utalii Zanzibar, Simai Mohamed Said ameeleza kwamba sera ya uchumi wa buluu inagusa matumizi bora ya bahari ambayo yatakua endelevu huku wakihakikisha bahari tuliojaliwa inakua salama.
Dar es Salaam. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohammed Said amesema sere ya uchumi wa buluu inagusa matumizi bora katika bahari, ambayo yatakua endelevu hivyo wananchi wanatakiwa kutambua umuhimu wa bahari, katika nyanja mbalimbali kama vile masuala ya uvuvi.
“Uchumi huu utakua endelevu ambapo kila mmoja atafaidika nao, wananchi na serikali wote kwa ujumla,”amesema.
Amesema jamii haitaweza kwenda katika uchumi wa buluu endapo watu watakuwa wanafanya uharibifu katika bahari, hivyo jambo hilo linatakiwa kuachwa mara moja.
“Kwa upande wa sekta yangu nataka tuhakikishe kwamba hii bahari, tuliojaliwa inabakia salama pamoja na viumbe vyote vilivyomo ndani yake,”amesema.
Hayo yalielezwa katika hoteli ya Crowne Plaza, iliyozinduliwa Novemba 25 yenye hadhi ya hoteli za kimataifa, ikiwa inapatikana Kisutu, jijini hapa.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa hoteli hiyo, Waziri Said amesema hoteli itatengeneza fursa kwa watu mbalimbali na kuwa kivutio kwa wenyeji na watalii wanaokuja Tanzania.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa hoteli hiyo Ravi Reddy ameeleza kwamba hoteli hayo itakuwa inahudumia watu wenye wadhifa mbalimbali, wakiwemo watalii, familia tofauti, wasafiri kutoka maeneo tofauti.
“Pamoja na hayo yote bado tunamikakati ya kutoa huduma nyingine na kutengeneza ajira kwa vijana mbalimbali,”amesema.
Mmoja ya wadau walihudhuria uzinduzi wa hoteli hiyo, Emiliana Stephen amesema anaamini hoteli iyo itafanya vizuri katika masuala ya utalii kutokana na huduma nzuri ambazo wahudumu wanazitoa.