Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Bashungwa amsimamisha kazi DED Muheza

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Innocent Bashungwa

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga (DED), Nassib Bakari Mmbaga kupisha uchunguzi.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga (DED), Nassib Bakari Mmbaga kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na Tamisemi leo Jumanne Agosti 30, 2022 imesema Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo sambamba na utendaji kazi usioridhisha.

Taarifa hiyo imesema Mmbaga amesimamishwa kazi kuanzia Jumanne ya Agosti 30, 2022

Waziri Bashungwa amewataka wakurugenzi wa halmashuri zote nchini kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu.