Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkenda aipigia chapuo chanjo ya Uviko-19

Waziri Mkenda aipigia chapuo chanjo ya Uviko-19

Muktasari:

  • Mbunge wa Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo nchini Tanzania,Profesa Adolf Mkenda amewataka wananchi wa jimbo hilo kutopuuza chanjo ya Uviko-19 na badala yake kuiamini Serikali na wataalamu wa afya ili kupunguza kasi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Mbunge wa Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo nchini Tanzania,Profesa Adolf Mkenda amewataka wananchi wa jimbo hilo kutopuuza chanjo ya Uviko-19 na badala yake kuiamini Serikali na wataalamu wa afya ili kupunguza kasi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Profesa Mkenda, ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Septemba 4, 2021 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mbomai, Kata ya Tarakea Motamburu,wilayani Rombo.

"Ugonjwa wa Covid-19 upo  na umeua sana hapa Rombo,tukichanja wengi tutaokoa na wengine ,mimi nimechanja,mke wangu amechanja na familia yote tumechanja, naombeni japo ni hiari mkachanje na Serikali sasa hivi imetoa fursa kwa wote, nendeni mkachanje,"amesema Profesa Mkenda

"Mkichanja nafasi ya kuambukiza na kuugua inakuwa ndogo, kama hujachanja unaweza kuugua sana na kuambukiza wengine, hebu fikiria hapo utakuwa umesababisha vifo vya watu wangapi ,"amesema Profesa Mkenda

 Amesema wapo baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakipuuza kuchoma chanjo hiyo licha ya wilaya hiyo kuathirika zaidi na vifo vingi vitokanavyo na ugonjwa huo na kwamba ni vema wakawaamini wataalamu wa afya na Serikali na kuchanja na kupuuza upotoshaji.

Mkuu wa Wilaya hiyo,Hamis Maiga,amesema mpaka sasa wananchi waliopata chanjo ni zaidi ya 2,000  na kwamba bado mwitikio ni mdogo huku akiweka wazi kuwa elimu zaidi inahitajika kuhamasisha wananchi kupata chanjo hiyo.