Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye VVU watakiwa kutoacha kutumia dawa

New Content Item (1)
Wenye VVU watakiwa kutoacha kutumia dawa

Muktasari:

Watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia matumizi ya dawa za kufubaza virusi hivyo na kuwa wazi ili kuushinda unyanyapaa.

Moshi. Watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia matumizi ya dawa za kufubaza virusi hivyo na kuwa wazi ili kuushinda unyanyapaa.

Rai hiyo imetolewa leo Jumanne Desemba mosi, 2020  na mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na VVU (Nacopha) , Leticia Mourice wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kitaifa inafanyikia katika viwanja vya shule ya msingi Mandela, manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema hali ya unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (VVU) katika jamii nchini bado iko juu na ili kuweza kuishinda changamoto hiyo ni muhimu watu wakawa wazi na kutumia dawa kwa usahihi.

"Ili kuushinda unyanyapaa ni muhimu kuanza dawa  kwa wakati, mara baada ya kupima na kugundulika na maambukizi ya VVU, lakini pia wazingatie matumizi sahihi ya dawa, hii itasaidia sana kuondoa unyanyapaa.”

"Pia ni muhimu kuwa wazi, kwani unapokuwa wazi katika jamii, kunakufanya uwe huru na amani ya moyo  na jamii itakuona wewe kama wengine, lakini pia itasaidia kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi,” amesema.

Amesema changamoto zilizopo, ni pamoja na  kuongezeka kwa maambukizi mapya kwa vijana walio katika umri wa kubalehe na kwamba vijana wa  kike wako kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi kutokana na kuwa kundi linalokumbwa na vishawishi vingi.

Amesema hali hiyo inachangiwa na sababu mbalimbali  ikiwemo  wazazi kutozungumza na vijana wao kuhusu  makuzi na athari wanazoweza kuzipata endapo wataingia katika vishawishi.

Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi mgeni rasmi ni waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.