Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wilaya ya Kishapu yaeleza mikakati yake ya usafi wa Mazingira

Ofisa mazingira wilaya ya Kishapu, Charles Kanwakabo akizungumza baada ya usafi.

Muktasari:

  • Halmashauri ya Wilaya hiyo imeanza rasmi mchakato wa ujenzi wa dampo la kisasa eneo la Sulagi huku kiwango cha usafi kikiwa asilimia 85.

Kishapu. Ofisa mazingira Wilaya ya Kishapu Charles Kanwakabo, amesema kiwango cha usafi kimefikia hali ya kuridhisha jambo linaloonyesha mafanikio makubwa kutokana na ushiriki wa wananchi, wanafunzi na viongozi mbalimbali kusafisha eneo hilo.

Akizungumza leo Julai 26, 2025 wakati wa zoezi la usafi wa pamoja lililofanyika eneo la Sulagi lililopo Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ameshukuru wote walihusika kwa namna moja au nyingine katika zoezi hilo,

“Kiwango cha usafi kikiwa asilimia 85, tunashukuru wananchi, viongozi na wanafunzi wa Kishapu sekondari kwa kushiriki kikamilifu, tunasisitiza kuwa usafi uwe sehemu ya maisha ya kila siku, si tu wa mwisho wa mwezi” amesema Kanwakabo.

Kwa upande wake, Mtendaji wa Mamlaka ya Mji mdogo Kishapu, Godwin Everygist amesema ujenzi wa dampo hilo ni sehemu ya mpango wa kuufanya mji wa Kishapu kuwa wa kisasa, ukiwa na miundombinu bora ya usimamizi wa taka.

“Katika kipindi hiki cha mpito, tunahimiza kila kaya kuhifadhi taka kwenye dampo la muda, dampo jipya la Sulagi litazalisha miji safi, salama na yenye ustaarabu wa mazingira na pia litakuwa suluhisho la taka holela” amesema Everygist.

Aidha, amesisitiza kuwa kila kaya inapaswa kuwa na choo bora na salama ili kudhibiti milipuko ya magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira.

Nao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kishapu akiwepo Petro Shambiti ameeleza baadhi ya changamoto zitakazo tatuliwa na uwepo wa dampo hilo ikiwa ni pamoja na utupaji taka hivyo unaopelekea magonjwa ya mlipuko,

“Tunashukuru kwa maamuzi yaliyofanywa ya kujenga dampo hili kwa sababu wengi wetu hatukuwa na sehemu maalum ya kutunza taka, wengi walitupa hivyo jambo ambalo lilipelekea magonjwa ya mlipuko kwa sababu ya uchafu” amesema Shambiti.

Zoezi la usafi limefanyika tarehe 26 Julai 2025, limehusisha maeneo muhimu kama vile Soko la Swalala, Uwanja wa Shirecu, na dampo la muda, miongoni mwa walioshiriki ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kishapu, walioonekana wakijitokeza kwa wingi, wakionesha uzalendo na mshikamano wa kijamii.