Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizara yafanya maboresho ya sheria kuinua mfuko wa Misitu

Wadau wa utalii wakiwa kwenye kikao cha kujadili tathmini ya mradi wa nyuki wachavushaji katika chuo cha usimamizi cha wanyamapori, Mweka. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya maboresho ya sheria ya misitu nchini ili kuwezesha mfuko wa Misitu katika kutekeleza shughuli za utafiti kwa wafugaji wa nyuki baada ya kuona sekta hiyo ikikuwa kwa kasi.

Moshi. Wizara ya maliasili na utalii imefanya maboresho ya sheria ya misitu nchini ili kuwezesha mfuko wa Misitu katika kutekeleza shughuli za utafiti kwa wafugaji wa nyuki baada ya kuona sekta hiyo ikikuwa kwa kasi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi msaidizi maendeleo ya ufugaji nyuki kutoka wizara ya Maliasili na Utalii, Daniel Pancras wakati walipokutana katika chuo cha usimamizi wa wanyamapori, Mweka kujadili na kufanya tathmini ya mradi wa nyuki ulioanzishwa na chuo hicho.

Amesema lengo la maboresho hayo ni kuweka msisitizo katika kuhakikisha sekta ya ufugaji nyuki inapata tafiti za kutosha na kukua kwa kasi hapa nchini.

"Serikali imeamua kufanya msisitizo mkubwa ili kuhakikisha sekta hii ndogo ya ufugaji wa nyuki inapata tafiti za kutosha, tafiti ambazo zinaenda kufanyika ni zile tafiti ambazo zitajibu changamoto zinazowakabili wafugaji wa nyuki hapa nchini na wadau wengine"amesema Pancras

"Sambamba na hilo baada ya kuhamisha shughuli za ufugaji nyuki kutoka Taasisi ya ufugaji ya wanyamapori (Tawiri) kwenda Taasisi ya misitu Tanzania (Tafori) tumeandaa mpango kabambe yenye kutoa mwongozo maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa tafiti za nyuki,"

Naye mratibu wa mradi wa  nyuki wachavushaji  kutoka chuo cha Mweka, Dk Emmanuel Martine amesema kuwa mwaka 2017 chuo hicho kilianza mradi huo ambapo mpaka kufikia sasa wameweza kupata aina mbalimbali za nyuki zipatazo 223 na kati ya hizo 17 zimerikodiwa nchini kwa mara ya kwanza.