Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PIRAMIDI YA AFYA: Matibabu salama ya mafua kwa watoto

Kutokana na hali ya hewa ya sasa ilivyo nimeona ni vizuri nikatoa ufahamu wa mafua kwa watoto hii ni kwasababu ndiyo kundi ambalo hupata wakati mgumu wanapougua ugonjwa huu wa mfumo wa hewa.

Mafua ni moja ya maradhi ya mfumo wa hewa ambayo mara kwa mara huwapata watoto wa chini ya miaka mitano na huweza kuugua mara tano hadi 10 kwa mwaka mmoja.

Watoto wa chini ya mwaka mmoja wakiwa na mafua huwa katika hali ngumu kwani kushindwa kunyonya vizuri.

Mzazi huwa na hofu kubwa anapoona mwanawe amebanwa na mafua na kikohozi.

Kama hatua za haraka hazitachukuliwa mwanzoni, baadaye huwa ni makaribisho mazuri kwa ugonjwa hatari wa homa ya mapafu (nimonia).

Wapo waliowahi kuniuliza maswali juu ya dawa za antibiotics na tiba ya mafua na kikohozi.

Si kila kikohozi au mafua yana hitaji kupewa dawa za antibiotic na si sahihi kujinunulia au kuandikiwa na mtu asiye tabibu au daktari.

Hatari ya kutumia kiholela dawa za antibiotic ni pamoja na kujitokeza kwa usugu wa bakteria dhidi ya dawa, kushusha kinga ya mwili na kuharisha sugu.

Zaidi ya asilimia 80 ya mafua ya kawaida husababishwa na virusi ambavyo havina dawa ya kuviua. Hupona yenyewe ndani ya wiki moja.

Virusi hawa ambao hushambulia tando laini za mifereji ya pua na kooni na mara nyingi virusi wa mafua huenea katika mfumo mzima na husababisha pia shambulizi la mirija ya hewa. Lakini ijulikane kuwa shambulizi la tishu za mapafu ndiyo husababisha homa ya mapafu, ugonjwa ambao unaongoza kusababisha vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano duniani.

Mafua pia husababishwa na mzio, kuvuta hewa chafu yenye vumbi, moshi unaokereketa kama wenye kemikali au sumu na hali ya hewa ya baridi na unyevu.

Uambukizi wa virusi vya mafua, bakteria, parasite ikiwamo minyoo na fangasi kwa watoto wenye kinga dhaifu hasa walio na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Kikohozi kisichozidi wiki mbili, mikoromo wakati wa kupumua, kupiga chafya, pua kuchuruzisha majimaji au kamasi, yanaweza kuwa yasiyo na rangi (ya virusi au mzio) na njano njano kijani (ya bakteria).

Dalili zingine ni joto la mwili kupanda, kushindwa kunyonya na kupumua vizuri, kulia na kutokuwa mtulivu, Matibabu salama ya mafua hukubalika katika miongozo ya matibabu ya WHO ya kupambana na mafua na kikohozi.

Watoto wanaonyonya waendelee kunyonyeshwa kipindi chote cha ugonjwa kwani maziwa ya mama kiasilia huwa na lishe yenye kinga inayomlinda dhidi ya maradhi.

Mtoto ambaye ameanza kutumia vyakula vya kulikiza ni vema ukatumia vitu kama chai na ukaidondoshea matone ya limao au machungwa na supu.

Machungwa, limao na ndimu huwa na vitamin C inayosaidia kufupisha dalili za mafua.

Hakikisha pia unampatia maji ya kunywa ya kutosha yasiyo baridi kwa ajili ya kuurudishia mwili maji. Katika hali ya ubaridi, tando laini za mfumo wa hewa hupoteza maji, kuupa mwili joto na hupunguza hali hii. Ni vema kutumia maji ya moto kumuogesha na kumkinga na baridi kwa kumvisha nguo zakutanda mwili mzima.

Msafishe na kitambaa safi kisichopukutisha pamba au nyuzi kufuta mafua yanayochuruzika na kuondoa taka zilizoganda puani.

Mpeleke mapema katika huduma za afya kama hatapata nafuu.