Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

STAKABADHI GHALAINI Ni mfumo mzuri ununuzi mazao ila vyama vya ushirika ni tatizo

Muktasari:

Mkulima wa korosho ameendelea kudhulumika licha ya Serikali kuweka mkakati wa kumuinua kiuchumi.

Stakabadhi ghalani siyo neno geni masikioni mwa Watanzania hasa, wanaoishi katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Singida, Kilimanjaro na Morogoro.

Wakati wakazi wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani wakiutambua mfumo wa stakabadhi ghalani kwa sababu ya zao la korosho, mfumo huo unatumika katika mkoa wa Singida katika zao la alizeti, Kilimanjaro kwa zao la kahawa na mkoani Morogoro kwenye zao la mpunga.

Huu ni mfumo wa kukusanya mazao pamoja kwenye ghala maalumu lililosajiliwa na Serikali kwa lengo la kuyauza kwa bei ya ushindani.

Katika mfumo huo, asasi za fedha zinaweza kutoa mkopo kwa dhamana ya mazao hayo yaliyohifadhiwa kwenye ghala na malipo ya wakulima yanafanywa baada ya mazao hayo kuuzwa.

Nyaraka kutoka Bodi ya Korosho Tanzania zinaonyesha kuwa, zao la korosho lilikuwa la kwanza nchini kuuzwa kwa kutumia mfumo huo.

Zinasema korosho zilianza kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani katika msimu wa mwaka 2007/2008 mkoani Mtwara na baadaye mkoani Lindi katika msimu wa mwaka 2008/ 2009.

Mikoa ya Ruvuma na Pwani ilianza kutumia mfumo huo wa stakabadhi ghalani katika msimu wa 2009/2010 na Mkoa wa Tanga ukaingia kwenye utekelezaji wake katika msimu wa 2011/2012.

Faida ya stakabadhi ghalani?

Kabla ya mfumo huo kuanza kutumika wafanyabiashara walikuwa wananunua korosho moja kwa moja kutoka kwa wakulima kupitia bei dira.

Katika utaratibu huo, wakulima walikuwa wakipunjwa malipo kutokana na ukweli kwamba wafanyabiashara walikuwa wakitumia vipimo vyao ambavyo vilifanya wakulima hao walipwe bei sawa au pungufu ya bei dira.

Bei dira ni nini?

Bei dira ni bei ya kujipanga kibiashara tu. Bei halisi hupatikana sokoni. Bei dira siyo mkataba kati ya chama cha msingi na wakulima. Wakulima hugawiwa fedha zao baada ya kulipwa kwa gharama za mauzo.

“Wakulima waliuza korosho zao kupitia vipimo visivyo rasmi kama vile kangomba. Katika utaratibu huo wakulima hawakuwa na uhakika wa soko la korosho na bei ya kuuzia korosho ilibadilika kila siku,” imeeleza taarifa hiyo ya Bodi ya Korosho Tanzania.

Mauzo ya korosho

Katika utaratibu wa stakabadhi ghalani, mkulima anapoweka mazao yake kwenye ghala, anakuwa bado anayamiliki mazao hayo mpaka yatakapopata mnunuzi wa mwisho.

“Kwa msingi huo, fedha za awali anazolipwa mkulima ni mkopo ambao unatolewa na benki kwa mujibu wa bei dira. Malipo halisi ya mkulima yanapatikana baada ya mauzo ya mazao yake kwenye chama kikuu cha ushirika na siyo hapo kwenye chama cha msingi,” inasema nyaraka hiyo ya Bodi ya Korosho na kufafanua;

“Hakuna mauzo yanayofanyika kwenye chama cha msingi wakati wa kukusanya korosho. Benki siyo mnunuzi wa korosho za wakulima, isipokuwa inawakopesha wakulima fedha kwa dhamana ya mazao yao yaliyoko kwenye ghala.”

Kwa mazao kwa pamoja?

Historia ya stakabadhi ghalani inaanza na dhana ya ushirika ambapo watu hujikusanya na kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kujiletea maendeleo endelevu.

Akiwasilisha mada katika warsha ya wadau wa Ushirika iliyofanyika mkoani Dodoma, Gloria Mazoko kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania anataja kazi za chama cha ushirika katika mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa ni pamoja na kukusanya mazao kutoka kwa wakulima.

“Upande wa korosho, chama hicho kina wajibu wa kuhakiki korosho hizo zikiwa kwenye madaraja, kufungasha korosho kwenye magunia kwa uzito sahihi na kusafirisha korosho hadi ghala kuu,” anasema.

Kazi zingine za chama cha ushiriki kwa mujibu wa Mazoko ni kuratibu mauzo na kuwagawia wakulima fedha zao baada ya mauzo.

Malipo ya awamu

Katika mfumo wa stakabadhi ghalani kanuni zinaeleza kuwa mnunuzi hulipia bei aliyoshinda kwa mkupuo mmoja hivyo kimsingi hakuna malipo ya awamu.

Anasema mfumo wa stakabadhi ghalani unatoa uhakika wa soko la korosho kwa wakulima na kuimarisha ubora wa korosho sokoni, hivyo kuifanya korosho hiyo iuzwe kwa bei ya ushindani badala ya bei ya dira pekee.

Mazoko anaendelea kueleza faida zingine za mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa ni kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi za korosho kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo ya tasnia ya korosho.

Stakabadhi ghalani pia hupunguza wimbi la madalali wanaonunua korosho na kutorosha kwa njia ya magendo.

Vyama vya ushirika ni tatizo

Ofisa Kilimo na Mifugo na Mtumishi wa Halmashauri ya Kilwa, Idara ya Kilimo, Maganga Salum anasema mfumo wa uuzaji wa stakabadhi ghalani ni mzuri ila usimamiaji ni tatizo.

Salum anasema vyama vimekuwa vikikiuka taratibu za stakabadhi ghalani kwa kumkata mkulima makato makubwa kuliko kiwango kilichowekwa.

Anasema taratibu zinavitaka vyama vya ushirika kukata Sh275.75 kila kilo kama ushuru kwa halmashauri na kufidia gharama mbalimbali.

“Mfano mwaka huu chama chetu cha ushirika kiliuza mnadani kilo moja kwa Sh1,590 kwa kilo lakini mkulima alilipwa Sh1,000 kwa kilo.

“Huu ni wizi kwa maana hata tukikadiria kwa makisio ya juu mkulima alikatwa Sh300, walikwa walipwe Sh1,290 kwa kilo. Huu ni wizi! Anaonya Salum.

Anasema vyama vya ushirika vimekuwa na historia ya ubadhilifu na licha ya kujikuta vinakufa na Serikali kutumia fedha nyingi kivifufua, vimekuwa kama kidonda ndugu, kwa kutozingatia masilahi ya wakulima.

Salumua anasema wakulima hutumia nguvu nyingi katika kuendeleza kilimo hicho lakini wamekuwa hawafaidiki kikamilifu. Matokeo yake ni kujikuta wakiendelea kuwa maskini.

“Naweza kusema kwa sasa hakuna mwelekeo wa kutekeleza lile lengo la kusukuma maendeleo ya nchi yetu mbele kwa kutumia vyama hivi,” anasema.

Umefika wakati kwa Serikali Kuu kukemea vikali wizi na ubadhirifu ndani ya vyama vya wakulima ambao.