Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Je, una kiu na ndoa yenye mafanikio?

Muktasari:

  • Kwa kuwa na ufahamu mkubwa. Ndoa inaweza ikajengwa kwa kufahamu sababu ya ninyi kuwa pamoja, ufahamu wa mambo yapi myazingatie kwenye ndoa yenu, nini mfanye na nini msifanye, yapi mambo hatari na yapi sio hatari. Je, unamfahamu mwenzako kwa kiasi gani na unafahamu nini utegemee kwa jinsia aliyonayo?

Watu wengi wamekuwa wakifundishwa na kuelewa kwamba tunachotakiwa kuwa nacho ili tuishi kwenye ndoa ni upendo peke yake. Upendo ukiwepo basi hakuna haja ya kingine chochote, mengine yatajijia yenyewe tu. Hiyo imekuwa ni nadharia potofu na wengi kwa kushindwa kuelewa wamepata shida kwenye ndoa zao. Hapa ninakupa nguzo nyingine muhimu zinazosaidiana na upendo katika kuidumisha ndoa au mapenzi yoyote. Yafuatayo ndio mambo yanayoweza kuleta mafanikio katika ndoa.

Ufahamu

Kwa kuwa na ufahamu mkubwa. Ndoa inaweza ikajengwa kwa kufahamu sababu ya ninyi kuwa pamoja, ufahamu wa mambo yapi myazingatie kwenye ndoa yenu, nini mfanye na nini msifanye, yapi mambo hatari na yapi sio hatari. Je, unamfahamu mwenzako kwa kiasi gani na unafahamu nini utegemee kwa jinsia aliyonayo?

Uelewa

Ni busara kuelewa mambo ya mahusiano kabla ya kufunga ndoa. Unapaswa kuelewa tabia ya rafiki yako, nguvu na udhaifu wake. Kuna vitu kwenye ndoa havihitaji majibizano yasiyo lazima, vinahitaji tu uelewa, ukiwa muelewa utapunguza misuguano isiyolazima, elewa haraka kile mwenzako anachotamani umuelewe, penye kuhitaji swali basi uliza ueleweshwe. Usijifanyishe umeelewa wakati haujaelewa.

Hekima

Hekima ni muhimu kwenye ndoa. Hii inakuwezesha katika kuamua vizuri kwa ustawi wa ndoa yako. Ni hekima ndio inakusaidia kufanya maamuzi yasiyo na majuto. Maamuzi ambayo yatazingatia ufahamu wako na uelewa wako.

Mapenzi/ upendo

Mapenzi yanapaswa kuwa jambo la nne la ndoa yenye mafanikio na sio la kwanza. Unapokuwa na uelewa, ufahamu na hekima basi upendo unakuja kuketi au kutuama sehemu salama kabisa. Ukiwa na upendo na hivyo vingine havipo basi utashangaa misuguano haiishi.

Ni vizuri ukajiuliza kabla ya kufunga ndoa “Ni kwa nini ninafunga ndoa?” “Nisababu zipi zinanifanya niingie kwenye ndoa?” usipojiuliza swali hili mapema na kulipatia majibu ya kiufasaha basi mbeleni baada ya kuoa au kuolewa unaweza kuja kujiuliza “Ni kwa nini nilifunga ndoa?” “Hivi kwanini nilioa au niliolewa?”

Bahati mbaya sana wakati unajiuliza maswali haya utakuwa umechelewa “it will be too late”. Ili kuwa na ndoa yenye mafanikio unahitaji ngazi tatu za mahusiano:-

Ngazi ya kwanza ya mahusiano ni Mungu/muumba

Hii ndio ngazi ya kwanza ya uhusiano na yemye umuhimu mkubwa sana, ngazi hii itaamua kiasi kikubwa cha uhusiano wako na wengine (wa karibu yako na wasio wa karibu yako).

Kumshirikisha Mungu katika kila tamanio la moyo wako. Zungumza na Mungu ni aina gani ya mume au mke unahitaji. Ni aina gani ya familia unayoitamani. Kuwa mwaminifu kwa Mungu kumwambia kila kitu kuhusu mume wako/ mke wako, mwambie kuhusu unachopendelea kama vile rangi, tabia, ngazi ya elimu na mengine yanayohusiana na hayo.

Wengi wetu husahau ngazi hii halafu tunapoingia kwenye ndoa kwa kukurupuka tunajikuta vitu vingi sivyo tulivyowahi kutamani na wala havikuwahi kuwa ndoto yetu hapo ndio kukata tama huja kwa kasi na kiu ya kutoka kwenye hiyo ndoa huanza.

Ndoa nyingi sana zimevunjika kwa staili hii. Tafiti zinasema wanandoa wenye mahusiano binafsi mazuri na Muumba wao huweza kuelewan, kuthaminiana na kuheshimiana kwa urahisi zaidi kuliko wale wasio na uhusiano huu.

Ngazi ya pili ya mahusiano ni familia

Familia ni muhimu sana wakati wa kutafuta mchumba. Uhusiano wa familia wenye nguvu utakusaidia kufanya maamuzi mazuri.

Kwa nini maamuzi mazuri ni muhimu? Hii ni kwa sababu, kuna tofauti kati ya maumivu kabla ya ndoa na maumivu ya kwenye ndoa. Ni bora ukaifahamu familia ya huyo mpenzi wako kwa kina ili kupunguza maumivu ya badaye.

Bora uumie sasahivi kwa vile utakavyovigundua kuhusu yeye au familia yako kuliko kuvinyamazia halafu vikakuletea maumivu makubwa kesho ukiwa kwenye ndoa tayari. Hakikisha unaifahamu familia ya rafiki yako, jua mahusiano yake na wazazi wake na ndugu zake.

Chunguza kama wana magonjwa ya kurithi, chunguza kama kunatabia z kifamilia, chunguza wazazi na ndugu wanavyomchukulia yeye, angalia ushirikiano wao katika mambo ya kifamilia, chunguza mambo yahusuyo imani zao pia.

Fahamu yeye ni mtoto wa ngapi na wako watoto wangapi na wajinsia gani. Taarifa hizi zitakusaidia sana huko mbeleni

“Utakayefunga nae ndoa anaweza kuwa na matokeo hasi au chanya katika mahusiano yako na familia yako. Baadhi ya migongano ya kifamilia huisha baada ya mtu kufunga ndoa na migogoro mingine huanza baada ya kufunga ndoa. Kwahiyo kuwa makini sana.”

Itaendelea...